BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WIZI WABUNI MBINU MPYA KUIBA FEDHA KATIKA MTANDAO WA WhastApp TANZANIA


Kumeibuka wizi mpya wa mtandao ambapo wadukuzi (Hackers) wanaweza kutumia namba yako ya WhatsApp kufanya uhalifu pasiwe wewe kujua hasa ukiwa Admin wa group ama mtu yoyote wataomuina anaweza kuibiwa.

Kuna njia ya kuweza kujilinda hasa kwa kuweka ulinzi katika simu yako (security code) katika namba yako uliyojiunga nayo WhatsApp ili isiweze kutumika mahala pengine popote (kujiunga WhatsApp kwenye simu nyingine) bila idhini yako.

Kitu unachoweza kufanya ili kuweka ulinzi kwenye namba yako, fuata hatua hizi yakupasa kufuata hatua hizi hapa chini.

Fungua WhatsApp yako
1) Nenda kwenye (settings)
2) Halafu kwenye (account)
3) (Two-step verification)
4) Ingiza tarakimu 6 za (security code)
5) Thibitisha tena hiyo (security code)
6) Ingiza e-mail ya kutumia pindi utakaposahau (security code) yako
7) Thibitisha tena hiyo e-mail.

Mpaka hatua hiyo utakuwa umeilinda namba yako kutumiwa na wadukuzi (Hackers) wa mtandao bila idhini yako.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment