BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

YANGA SC YAPOTEZA MCHEZO WA NUSU FAINALI MICHUANO YA SPORTPESA CUP 2017 KWA MIKWAJU YA PENALTI DAR ES SALAAM

Klabu ya Yanga SC ya Tanzania imesambaratishwa na kuondoshwa katika mashindano ya Sportpesa Cup 2017 baada ya kufungwa bao 4-2 mbele ya AFC Leopard ya Kenya katika mchezo mkali wa nusu fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kufuatia suluhu ya 0-0 ndani ya dakika 90.

AFC Leorpad katika mchezo huo walifanikiwa kupata penalti nne huku wakikosa mmoja wakati Yanga SC wakipoteza mbili na kujikuta timu zote za Tanzania zikiaga michuano hiyo.

Klabu nyingine zilizoaga mashindano hayo ni pamoja na Simba SC iliyochapwa bao 5-4 nayo ikiondoshwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti wakati Singida United nayo iliaga kupitia changamoto ya mikwaju ya penalti.


AFC Leopard imekuwa timu ya kwanza kutinga fainali huku ikishubiri mshindi kati ya Nakuru Star FC iliiyoitoa Simba itayochuana katika mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi Goal Mahia zote za Kenya.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment