BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ALIYEMUUA AFISA WA JESHI LA POLISI AKAMATWA

Kisa cha mshukiwa mmoja wa mauwaji nchini Japan, kimethibitisha kuwa, unaweza kukimbia kwa miaka mingi, lakini hutaweza kujificha daima, kwani siku moja utakamatwa.

Mwanamapinduzi wa mrengo wa kushoto Masaaki Osaka, amekamatwa na kuhukumiwa kwa kosa la kumuuwa afisa mmoja wa polisi, wakati wa maandamano yaliyofanyika katika barabara za mji mkuu Tokyo, miaka 45 iliyopita.

Anadaiwa alimchoma moto afisa huyo kwa bomu la petroli la kujiundia maarufu kwa jina Molotov Cocktail petrol bomb.Masaaki Osaka amekuwa akisakwa na polisi tangu mapema miaka ya 1970s

Hakuna mshukiwa wa uhalifu amewahi ambaye amehepa vyombo vya usalama kwa muda mrefu kiasi hicho, vyombo vya habari nchini Japan vimeripoti.

Serikali ya Japan haina hukumu ya kifo, kifungo kirefu cha miaka 15 kilifutiliwa mbali mwaka 2010.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment