BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

YERCKO NYERERE YAMKUTA YA KUMKUTA BAADA YA KUKAMATWA POLISI NA KUFIKISHWA MAHAKA DARMANI

Mfanyabiashara Yericko Nyerere

Dar es Salaam.
Mfanyabiashara Yericko Nyerere amefikishwa leo (Ijumaa) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupandishwa kizimbani akikabiliwa na kesi nyingine ya kuchapisha maneno yenye nia ya uchochezi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.

Akisomewa shtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage, Yericko anadaiwa kuwa Mei 28, 2017 kwa nia ya kuwachochea Watanzania alichapisha maneno kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook yasemayo:

“Maazimio ya Baraza Kuu yalikuwa (1) Katiba Mpya, (2) Tume Huru, (3) Bunge, (4) Haki ya Kikatiba ya kuishi (Ben Saanane), (5) Haki ya Kikatiba ya kukutana na kuzungumza (Mikutano ya Hadhara ya Kisiasa) Hayo ndiyo yatahubiriwa katika Operesheni Ukuta.

Baraza Kuu limeridhia kwa kauli moja kwamba vita rasmi ya kulikomboa Taifa imezinduliwa na kama wewe Mtanzania unaogopa kulitetea Taifa hili ni bora uka kaa kando, nenda huko CCM ambako michemsho na supu vipo kwa wingi…kufa kwetu ni ukombozi wa Tanzania….” Mwisho wa kunukuu.

Yericko ambaye anatetewa na Wakili Peter Kibatala baada ya kusomewa shtaka hilo amekana na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wake bado haujakamilika. 


Hakimu Mwijage amemtaka mshtakiwa huyo kuwa na mdhamini mmoja ambaye amesaini hati ya dhamana ya maneno ya Sh10 milioni, amekamilisha na kuachiwa huru. 

Kesi imeahirishwa hadi Julai 6, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia upelelezi utakuwa umekamilika ama la./Mwananchi
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment