BUNGE LAPITISHA MISWADA MIWILI YA SHERIA, MIKATABA YA MALIASILI
Wabunge wamejadili na kupitisha miswada miwili ya sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu masharti hasi katika mikataba ya maliasili za nchi wa mwaka 2017 na mswada wa sheria ya mamlaka ya nchi kuhusiana na umiliki wa 7/3/2017.
Miongoni mwa yaliyomo katika miswada hiyo ni pamoja na ushirikishwaji wa wananchi katika umiliki wa rasilimali za nchi, uzuiaji wa usafirishaji wa rasilimali nje ya nchi kabla ya kuongezwa thamani.
Mashauri kati ya mwekezaji na serikali kutopelekwa mahakama za nje na badala yake kutafutiwa ufumbuzi katika mahakama za hapa nchini lakini pia wawekezaji kuhifadhi fedha zao katika benki za hapa nchini.
Suala lingine ni kulipa nguvu Bunge kupokea taarifa zote za mikataba ili kujiridhisha kama lina maslahi kwa wananchi na kama sivyoitarudishwa kwa serikali ili kutengenezwa upya.
Kamati ya pamoja iliyoteuliwa na Spika na kupewa jukumu la kuichambua miswada na kupokea maoni ya wadau imeshauri serikali iharakishe ujenzi wa mitambo ya uchakataji wa rasilimalighafi ili wawekezaji wapate huduma hiyo nchini.
Kuboresha mahakama kutoa haki yanapotokea matatizo na pia serikali itunge haraka kanuni zitakazotokana na miswada hiyo kuruhusu utekelezaji mapema huku kambi rasmi ya upinzani bungeni ikidai utungwaji wa sheria kwa hati ya dharula hakutoisaidia nchi kunufaika na rasilimali zake
Wakijadili miswada hiyo katika mjadala ambao ulimlazimu naibu spika kusimama kila wakati kutoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo wametaka sheria kutamka ulazima wa watu waishio pembezoni mwa migodi kunufaika kutoka kwa makampuni ya uwekezaji tofauti na sasa kuonekana kama hiari. Chanzo ITV
0 comments:
Post a Comment