BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ESTER BULAYA AIBUKA KIDEDEA KATIKA MAHAKAMA YA RUFANI

Dar es Salaam. Mahakama ya Rufani imetupilia mbali rufaa dhidi ya Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya.

Hukumu ya rufaa hiyo imesomwa leo Julai 28 na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Elizabeth Mkwizu.

Wapiga kura hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Escietik Malagila walikata rufaa mahakamani hapo wakipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, iliyompa ushindi Bulaya katika kesi ya uchaguzi waliyoifungua wakipinga matokeo yaliyompa ushindi Bulaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Rufaa hiyo ilisikilizwa Mei 11 mwaka huu na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani. 


Akisoma hukumu hiyo Naibu Msajili Mkwizu amesema kuwa hoja za warufani hao hazina msingi kwani kasoro walizokuwa wakizilalamikia hazikuwa na athari katika matokeo ya uchaguzi huo.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: