BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YAWAPIGIA MAGOTI WAFUGAJI ILI KUMALIZA MIGOGO

Arusha. Serikali imewaomba viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania na watetezi wa haki za wafugaji, kuhakikisha wanaondoa migogoro na wakulima ambayo imekuwa ikijitokeza na kurudisha maendeleo nyuma.

Akizungumza jijini hapa jana, katika ufunguzi wa warsha iliyowakutanisha watetezi wa haki za wafugaji nchini, Katibu Tawala Wilaya ya Arusha, David Mwakiposa alisema lengo ni kuwajengea uwezo waweze kuondoa migogoro.

“Serikali tunaomba watetezi wa haki za wafugaji kuangalia kwa uzito wa kipekee kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima, wahamasishe uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata bidhaa za mifugo ili kumuunga mkono Rais John Magufuli katika sera ya viwanda,” alisema Mwakiposa.

Mwakiposa alisema sekta ya wafugaji na kilimo inaajiri zaidi ya asilimia 70 ya wananchi, ndiyo sekta pekee ambayo haihitaji elimu kubwa tofauti na ajira za viwandani na sehemu nyingine, hivyo ni muhimu kujengwa uwezo.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa alisema ni vizuri wakajengewa uwezo katika sera, sheria na mifumo ya utoaji haki katika Taifa na nje ya nchi ili waweze kutetea vizuri wafugaji.

“Tunaamini watetezi hawa wakifahamu vizuri sera na sheria wataweza kuangalia mifumo ya utoaji haki kama haitendeki, kwa wafugaji wataweza kutumia fursa hiyo kuwatetea vizuri,” alisema.

Katibu wa chama cha wafugaji nchini, Maghembe Makoye alisema Tanzania ina mifugo mingi hivyo ni muhimu wahusika wa sekta hiyo kujengewa uelewa na kujielekeza kuunda mabaraza ya usuluhishi ngazi za vijiji, kata, tarafa hadi wilaya ili kuhakikisha kundi hilo haligombani. 


“Ni vizuri tukihamasishana kufuga kisasa ili kujiongezea tija katika uzalishaji wa bidhaa za wafugaji na kupata masoko ndani na nje ya nchi,” alisema.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: