BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIGOGO WA UHAMIAJI ASIMAMISHWA KAZI KWA KUWAPA VIBALI VYA KUISHI TANZANIA WASOMALIA 50


Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Grace Hokororo, aliyesimamishwa kazi na Rais Dk Joh Pombe Magufuli.

RAIS, Dk John Magufuli amemuagiza Waziri, Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Grace Hokororo kwa tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi kinyume cha taratibu.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa Uhamiaji kwenye makao makuu ya idara hiyo jijini Dar es Salaam. Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali vya uraia nchini.

Alisema haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.

“Idara ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali kuingia bila kufuata taratibu,” alisema na kusisitiza kuwa, ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini ukweli.

Alisema serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya ya uingiaji raia mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu, hivyo Rais Magufuli ameagiza Ofisa huyo asimamishwe kazi na uchunguzi ufanyike ili kubaini malengo yake.

“Hawa Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini wameingia tu na kupewa vibali, hivyo Mheshimiwa Rais Dokta John Magufuli ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe kujua ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao,” alisema.

Pia Waziri Mkuu ameiagiza idara ya Uhamiaji, wadhibiti kitengo cha utoaji hati za kusafiria za Kibalozi na kwa wanaomaliza muda wasipewe tena. 


“Lazima hati hizo zikaguliwe katika mipaka yote na maeneo yote ya usafiri ili kujua kama huyo anayeitumia bado ana hadhi hiyo na msiporidhika ichukueni, kwani kuna watu wanazitumia vibaya,” alisema.

Hata hivyo, Waziri Mkuu aliagiza uchunguzi wa kina ufanyike kwa watu wote walioomba hati za kusafiria pamoja na vibali vya makazi, kama wanakidhi matakwa ya kisheria kabla ya kuwakabidhi.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment