BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MUVEVENI NA DK MAGUFULI KUKUTANA USO KWA USO JUMAMOSI KATIKA TUKIO LA KIHISTORIA


Rais Dk John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni

RAIS John Magufuli na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Jumamosi ijayo wanatarajiwa kuweka jiwe la msingi la mradi mkubwa na wa kihistoria wa bomba la kusafi risha mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga.

Mradi huo ni moja ya miradi mikubwa ambayo Tanzania, imeipata na kuanza kutekelezwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani Novemba 5, 2015. 


Kwa mujibu wa taarifa ya jana ya Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, uwekezaji wa mradi mkubwa huo ni wa Dola za Marekani bilioni 3.5 (takribani Shilingi trilioni 8 za Tanzania).

Urefu wa bomba hilo ni wa kilometa 1,445 na kati ya hizo, kilometa 1,115 zitajengwa Tanzania na mafuta ghafi yanayotarajiwa kusafirishwa kwa siku ni mapipa 216,000. 


“Inatarajiwa wakati wa ujenzi wa mradi huu, ajira takribani 10,000 zitazalishwa na Watanzania watakuwa wanufaika wakubwa wa ajira hizi.

Nchi zetu za Tanzania na Uganda zitapata manufaa makubwa ya kiuchumi kutokana na kodi na tozo mbalimbali, mrahaba na shughuli nyingine za kibiashara zitakazoambatana na mradi huu.

“Nachukua fursa hii, kuwaalika Watanzania wote kufuatilia matangazo ya moja kwa moja yatakayorushwa na vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kwa siku hiyo ya sherehe za uwekaji jiwe la msingi na pia kufuatilia matangazo mbalimbali na machapisho yatayotolewa na vyombo vyetu vya habari na mitandao ya kijamii kuelekea siku hiyo,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment