BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MACHACHE KUHUSU HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

Na Geofrey Chambua
Huwezi andika hstoria ya Muhi2 bila kutaja jina la Sheikh Sewa Hadji Paroo, mwana jamii ya Ismailia mzaliwa wa Zanzibar.

Sewa Haji Paroo Alifika Zanzibar Akitokea Ktk Miji Ya Bhuj Na Kutch Na Mnamo Mwaka 1852 Alifungua Duka La Bidhaa Mbalimbali Huko Zanzibar, Mnamo 1860 Akafungua Duka Lingine Kubwa Bagamoyo Na Kuweka Makazi Yake, Biashara Zake Zikawa Kubwa Na Kuwa Tajiri Mkubwa Sana, Alisaidia Watu Wote Bila Kujali Rangi, Dini Wala Kabila Zao, Alinunua Majengo Mengi Na Kuyafanya Maeneo Ya Watu Wasiojiweza, Alijengaja Mashule Na Hospitali Kadhaa ktk Mji Wa Mzizima (Leo Inaitwa Dar es Salaam).

Awali Sewa Hajj ambaye ni muajemi alijenga Hospitali ya kwanza kubwa katika Tanzania, ilikuwa inaitwa kwa jina la Sewa Haji, ambayo ilikuwepo kabla ya uhuru katika eneo kati ya Kituo cha sasa cha Kati cha Polisi na Ofisi ya Kituo Kikuu cha Usalama Barabarani, jijini Dar es Salaam, ikitpa matibabu 'BURE'

Baadaye wakati uhuru unapatikana, Sewa Haji, ikahamishiwa pale ambako sasa ni Muhimbili, lakini wakati huo ilikuwa inajulikana kuwa Princes Margaret Hospital, kwa heshima ya Malkia wa Uingereza wakati huo kwani majengo mengi yalijengwa kwa hisani/ufadhili wake.

Sewa Haji pia ndiye mwanzilishi wa Shule ya Msingi Mwambao Bagamoyo (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amesoma shule hii) na Hospitali ya Bagamoyo.

Mnamo 1963 Iliitwa Muhimbili Hospital, Na Mojawapo Za Wodi Inaitwa SEWA HAJI,

JE WAJUA ASILI YA JINA MUHIMBILI ?
Neno Muhimbili limetokana kwa kizaramo "mibili" likimaanisha kiungo cha mtoto tumboni na mama yake (plasenta) Hospitali ilipoanza wazaramo walisema "hapo ndipo wanawake wanapoenda kuacha mibili yao". Neno Muhimbili likazaliwa nalo ladumu hadi leo.

Wadi nyingine hapo Muhimbili zimeenziwa majina ya wanaenzi kama vile Kibasila NA Mwaisela

Kibasila alikuwa Pazi (chifu) wa Wazaramo maeneo ya Magogoni/Mzizima (kama kuna watu wanaoijua hiyo sehemu). Maeneo ya siku hizi ni Wizara ya Utumishi na Ardhi.

KIBASILA alinyongwa na Wajerumani kutokana na msimamo wake wa kukaidi kutawaliwa na Wazungu hao! Alinyongwa kwa kamba kwenye mti wa mwembe katika eneo ambalo sasa kinajengwa Kituo cha Mabasi yaendayo kasi, (Kamata, karibu na duka kubwa la Shoprite, barabara ya Nyerere). 


Tusisahau historia hii muhimu! Kwa kuisahau ndiyo maana hatujiamini na sasa tunatawaliwa tena kiuchumi na hawa Wazungu!

Mwaisela
Dr E.F Mwaisela alikuwa Daktari Mwanaharakati aliyepigania sana maslahi ya madaktari wazawa

*As late as 1940s people like Dr. E.F. Mwaisela, when petitioning about the incommensurable remuneration they received, based their arguments on the education status and the life situation expected form them.

Dr MWAISELA alikuwa ni daktari bingwa wa mwanzo nwenye asili ya Kiafrika nchini mwetu.


yapo baadhi ya mabweni yamepewa majina ya Mwaisela Samson Mwamanda huenda anayajua ya kule Rungwe SEKONDARI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: