BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MADIWANI WA CCM WASUSIA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI MBELE YA CHADEMA


Madiwani wa CCM, wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wamesusia kikao cha Baraza la halmashauri hiyo baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa madiwani wa Chadema kumkataa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Esther Mmasi kuhudhuria kikao hicho.

Hatua ya kumkataa mbunge huyo ilieelezwa kuwa ni kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo vya halmashauri, jambo ambalo lilielezwa kuwa amepoteza sifa za udiwani.

Kikao hicho ambacho kilifanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo kilivunjika wakati wajumbe wakipitia muhtasari wa kikao kilichopita, baada ya kuona jina la mbunge huyo likiwa katika orodha ya waliotoa taarifa ilhali mwenyewe akidai hakuwa na taarifa ya kikao hicho.

Hoja ya kukataliwa kwa mbunge huyo ilitolewa na Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Diwani wa Ivaeny, Elia Kiwia alipohoji uhalali wa mjumbe huyo kuhudhuria kikao hicho wakati amepoteza sifa za kuwa diwani.

“Mwenyekiti, kanuni za halmashauri yetu kifungo cha 69 (e) kinaeleza kuwa mjumbe yeyote yule bila sababu ya kuridhisha au bila idhini au kibali cha maandishi cha mwenyekiti anayekosa kuhudhuria mkutano mitatu ya kawaida inayofuatana au kamati ambayo yeye ni mjumbe anapoteza sifa,” alisema Wakili Kiwia.

Naye Diwani wa Kirua, Robath Mrisho alisema mjumbe hastahili kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao tangu alipoapishwa mwisho mwa Desemba 2015.

Hata hivyo, Diwani wa Orkolili (CCM), Jonathan Nasari aliwataka madiwani kuliangalia suala hilo kwa umakini kutokana na wabunge wengi kushindwa kuhudhuria na mwingiliano na vikao vya bunge.

Akijitetea, Mmasi alikiri kutokuhudhuria vikao kutokana kutopatiwa barua za wito wa vikao na mkurugenzi. Kufuatia mvutano huo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Frank Tarimo aliamuru kuondoka kwa mbunge huyo ili kuendelea na kikao lakini wenzake wa CCM walitoka nje.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: