MAMBO YA KUFAANYA ENDAPO UTAKUTANA NA TEMBO ILI KUJINUSURU NA KIFO.
Tembo ni mpenzi wa kula, hutumia chakula zaidi ya kilo 130.
Ana akili nyingi mno, baadhi ya mambo hufanya kwa ustadi kama wanavyofanya binadamu mfano;
(a) Wanapokutana wana namna yao ya kusalimiana, kwa kuinua mkonge wao.
(b) Ana kumbukumbu mno, anaweza kukumbuka tukio hata la mwaka mmoja uliopita, kwahiyo usijemfanyia ubaya sehemu ukafikiri atakusahau. Wanyama ambao hufanya matukio ya kukamata mtoto wake, huwaweka katika kumbukumbu na kila wanapokutana huwa ni ugomvi mwanzo mwisho.
(c)Hupenda kuoga kila anapokutana na maji, hapendi kunuka harufu ambayo hunuka viumbe wa jamii yake kama nyati. Kwa kutumia mkonga wake hujimwagia maji mengi kujiweka safi.
(d)Wana lugha ya mawasiliano kama bianadamu ambapo hufanya mawasiliano kwa kugusana, ishara pamoja na kuunguruma.
(e)Wanapokuta tembo mwenzao kafa, hukusanyana na kufanya msiba ambapo majike hutoa machozi kabisa na husimama eneo hilo kwa saa kadhaa kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuufunika mwili wa mwenzao huyo kwa miti na majani.
3. Ndio mnyama pekee ambaye anaweza akafa akiwa amesimama na watu mkajua ni mzima.
4. Mletee mzaha wowote yeye lakini usimchezee mwanawe, ana mapenzi ya kweli.
Anapovuka sehemu ambayo ina barabara ambayo hupita viumbe wengine pamoja na magari, hutangulia umbali kiasi kisha huenda kukaa katikati ya barabara mpaka hapo mwanawe atakapovuka, kwahiyo nyie na magari yenu ni jukumu lenu kusubiri mtoto wake avuke wakati mkiwa mmesimamisha gari zenu, ole wako ukaidi au upige honi au ulete jeuri yoyote.
Huweza kuelewa lugha ya mwanadamu kwa kusoma ishara ya mwili wake pindi anapoongea, mfano akivamia mashamba ya wanadamu wanapotokea na kuanza kupiga kelele hutambua kuwa wanatangaza ubabe hivyo hufanya balaa ambalo huisha akiwa amekumaliza kabisa.
7. Akianza kukimbia kadri anavyokwenda mbele ndio huongeza spidi, kwa sababu mwili wake hujichochea zaidi akiwa katika mwendo.
8. Hawezi kukimbia umbali mrefu, kama ilivyo kwa wanyama wepesi.
9. Hutumia vichuguu vikubwa katika kujikuna sehemu zinazowasha, kwa sababu ndio hugusa sehemu kubwa ya mwili wake, lakini inapokosekana mti ndio huwa mbadala japokuwa huchubua ngozi zao.
10. Anatumia saa nne kulala, hupendelea zaidi kusimama, kwa sababu akilala kuamka huwa shughuli, hutumia muda kidogo kuutingisha mwili wake ili aweze kuamka, kwa kifupi hawezi kusimama ghafla.
11. Wanapotembea watoto hupewa ulinzi maalumu kutokana na mazingira, wakati wote mama hutangulia mbele na dume huangalia upande wa kukaa kulingana na sehemu wanayopita ina wanyama wa aina gani wanaowinda.
12. Bado hajatokea mnyama mwenye uwezo wa kumdondosha tembo, tena si mzee tu bali hata kijana. Simba na nguvu zake zote hata wakiwa sita hawawezi kumpeleka chini.
Ukikutana naye ufanye nini?
Bahati nzuri ni kwamba tembo si mnyama mkorofi, unavyokuja ndivyo anavyokupokea. Hivyo, kukuumiza au kutokuumiza ni namna atakavyokuwa ameona inafaa, unapokutana naye tambua ya kwamba ni mnyama asiyependa kelele kabisa.
Tembo hupenda mno kuheshimiwa katika uamuzi anaofanya iwe unakukera au vinginevyo, ukikaidi unaweza kugharimu maisha yako.
Pamoja na uzito mkubwa alionao, si rahisi kumshinda mbio akiamua kukukimbiza, anapokimbiza huongozwa na harufu zaidi kwakuwa macho yake hufunikwa na masikio, ili uweze kumpoteza kwa urahisi inakupasa ukimbie kwa kuufuata upepo unakoelekea ili harufu yako.
Ili isiweze kumfikia kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na kukata kona za mara kwa mara kwakuwa humchukua muda kidogo mpaka aweze kugeuza mwili wake, mpaka afanikishe zoezi hilo hata mwendo wake hupungua.Mtanzania
0 comments:
Post a Comment