BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA YA MATUKIO MBALIMBALI MANISPAA YA MOROGORO JULAI 2017


Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wakiwa katika foleni kubwa ya kulipia kodi ya jengo mwishoni mwa wiki katika ofisi ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika barabara ya stehseni katika zoezi lililokuwa limefikia mwisho Juni 30 mwaka huu lakini kutokana na idadi kubwa ya kukosa kulipia kodi hiyo serikali imelazimika kuongeza wiki mbili/PICHA ZOTE NA JUMA MTANDA.Askari kanzu kushoto akiwa amemshika kijana Samuel Malisheli (Baba Kaila) kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu uporaji wa simu za mkononi kwa kutumia pikipiki katika mitaa mbalimbali ya manispaa ya Morogoro wakati akimpeleka kituo kikuu cha polisi cha mkoa huo.

Mwakilishi wa sheikhe wa jumuiya ya mabohora mkoa wa Morogoro, Zoharbhai Rampurwalla akipanda mche wa mti kando ya hifadhi ya mto Morogoro ambapo jumuiya hiyo ilipanda michezo 25 aina ya mkangazi ili kukabiliana na changamoto za uhalibifu wa mazingira na tabianchi na kutoa msaada wa vyakula kwa wazee wa kambi ya Fungafunga iliyopo kata ya Kichangani mkoani hapa.

Mkurugenzi msaidizi ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu, Andrew Mwalwisi akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa makatibu wamabaraza ya wafanyakazi, viongozi wa Tughe sehemu za kazi na waajiri inayofanyika kwa siku tatu mkoani Morogoro.

Mkufunzi wa mafunzo ya matumizi ya maktaba kwa wakutubi na wanafunzi shule za msingi kutoka shirika la maendeleo la Korea (KOICA), Ja Young Lee (katikati) akiendesha mafunzo hayo mbele ya wanafunzi wa shule za msingi, kulia ni Mkutubi mkuu maktaba ya mkoa Morogoro, Edward Fungo na kushoto ni Mkutubi msaidizi wa maktaba hiyo, Mashaka Nyama.
Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wakifua nguo katika mto Morogoro eneo la Fungafunga kama walivyokutwa, mwanzoni mwa mwaka huu Morogoro ilikumbwa na ukame uliosababisha mto huo wenye asili ya kutiririsha maji masika na kiangazi kukauka kutokakana uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment