BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MATAJIRI WAKUMBWA NA KASHFA YA KUSAFIRISHA BINADAMU

Usafirishaji haramu wa binadamu duniani umetajwa kuwa tatizo lenye uhusiano wa karibu na biashara ya dawa za kulevya kwa sababu inafanywa na watu wenye nguvu ya fedha.

Wadau mbalimbali walisema hayo jana katika Maadhimisho ya Siku ya Kupinga Usafirishaji Haramu wa Binadamu yaliyoandaliwa na Shirika la Kidini la Mabinti wa Immaculate (DMI).

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, James Mkumbo alisema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014 zilizotolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) utumikishwaji watu kazi za lazima bila hiyari yao huwaingizia faida wafanyabiashara hao Dola 150 bilioni za Marekani kwa mwaka.

Mratibu wa DMI, Sista Lawrance Inigo, alisema tatizo la usafirishaji binadamu ni kubwa hasa kwa watoto na kwamba juhudi za pamoja zinahitajika kukabiliana nalo.

Mwanasheria Dotto Joseph alisema: “Wahusika wa biashara hii ni watu wakubwa na wenye fedha.”

Joseph alisema ni kosa la jinai kwa mtu kuwa dalali wa kusafirisha watu na kwamba ifike wakati hata kampuni zinazotoa nafasi za watu kwenda nje ya nchi kusoma zichunguzwe.

Diwani wa Mbezi, Hamphrey Sambo alisema wananchi, Serikali na viongozi wa dini wanawajibu wa kukemea biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu. 


Alisema migogoro na mizozo ya kibinadamu huwaweka watu katika hatari zaidi ya kusafirishwa kwa ajili ya kunyanyaswa.Mwananchi
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment