BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MGOGORO: SERIKALI KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA KYELA-MBEYA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewapa siku mbili madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya, kumaliza tofauti zao zina zokwamisha utendaji wa Halmashauri hiyo na kuendelea kufanya kazi walizotumwa na wananchi.

Tofauti hizo ambazo zimedumu kwa takribani mwaka mmoja, zimesababisha madiwani hao kushindwa kufanya vikao, jambo linalokwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi katika halmashauri hiyo.

Alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya. 


Alisema ikifika kesho madiwani hao wawe wamemaliza tofauti zao na wawaite wakuu wa idara na kuwapa taarifa hiyo ili shughuli za maendeleo, ziendelee kutekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo.

“Baraza la Madiwani limegawanyika, mna mgogoro tunataka uishe na mshirikiane na mshikamane katika kufanya shughuli za maendeleo ili wananchi waweze kupata manufaa. 


Mkiendeleza migongano hatutawavumilia Serikali ina uwezo wa kulivunja baraza,” alisema.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment