BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANAMUZIKI WA MSONDO NGOMA SHABAAN DEDE AAGA DUNIA HOSPITALI YA MUHIMBILI


Hizi ni habari mbaya kwa mashabiki wa Msondo Ngoma Music Band, Mwimbaji na mtunzi tegemeo wa bendi hiyo Shaaban Dede amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Mwanamuziki mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia leo Alhamis Julai 6, 2017 saa mbili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu kwa takriban wiki mbili, mwanae Hamad Dede amethibitisha.

Hamad Dede amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es salaam, na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara zitapokamilika kupangwa.

Marehemu Dede atakumbukwa kama mmoja wa wanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania kwa sauti yake tamu na utunzi wa nyimbo mbalimbali zilizoshika chati akiwa na bendi mbalimbali zikiwemo Tabora Jazz, Bima Lee, Mlimani Park na Mondo Ngoma ambako alikuwa anatumikia hadi maiti yamemkuta. Chanzo-Michuzi blog
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment