BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RUFANI YA GODBLESS LEMA YA KUMTUSI MKUU WA MKOA ARUSHA YASHINDIKANA


Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

RUFANI ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na mkewe Neema katika kesi ya kumtukana Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo, ilishindikana kusikilizwa jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na kuahirishwa hadi Septemba 19.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda hiyo, Angelo Rumisha alisema sababu za kuahirisha rufaa hiyo ni Jaji Salma Maghimbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha aliyepangwa kuisikiliza kuwa likizo.

Wakati kesi hiyo ikiahirishwa, Lema ambaye anahudhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma hakuwepo mahakamani hapo. Neema alihudhuria.

Lema na Neema wapo mbele ya Jaji Magimbi wakipinga kesi ya kudaiwa kumtukana Gambo isisikilizwe na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kwa kuwa wameshtakiwa kwa sheria ya makampuni wakati wao siyo kampuni.

Aidha, Lema na mkewe wanapinga kusikilizwa kwa kesi hiyo kwa kuwa hati ya mashitaka imejaa makosa na kukataa Hakimu Nestori Barro kuruhusu kurekebisha makosa yaliopo kwenye hati ya mashitaka ili kesi iendelee.

Awali, wakili wa Mbunge huyo, Sheck Mfinanga alisema washitakiwa wanashitakiwa kwa Sheria ya Mawasiliano ya Kielekroniki na Posta, ambayo kimsingi haiwahusu watu binafsi bali makampuni makubwa ya simu na vyombo vya habari.

Pia Mfinanga alisema sheria inayowabana washitakiwa mmoja mmoja ni Sheria ya Makosa ya Kimtandao.

Hakimu Barro alikuwa amesema ingawa hati ya mashitaka imekosewa, ingeweza kufanyiwa marekebisho wakati wowote kwa mujibu wa sheria na kutaka kesi hiyo iendelee na mashahidi waliopo.

Katika kesi ya msingi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, upande wa Jamhuri una mashahidi watano ambao ni Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO), George Katabazi, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Damasi Massawe, mhusika kutoka kampuni ya simu ya Vodacom pamoja na mtaalam wa picha.

KAMA UARABUNI
Vielelezo vinavyotarajiwa kutolewa katika mashitaka hayo ni nakala ya taarifa za mawasiliano ya simu kutoka kampuni ya Vodacom, simu ya mke wa Lema pamoja na taarifa ya uchunguzi kutoka kitengo kinachoshughulikia masuala ya kiuchunguzi (Forensic Bureau).

Awali akiwasomea maelezo ya kesi hiyo, Wakili wa serikali, Amina Kiango alidai kuwa Godbless Lema na mke wake Neema, Agosti 20 mwaka jana, ndani ya Jiji la Arusha, walimtumia ujumbe wa simu ya kiganjani wenye lugha ya matusi Mkuu huyo, huku wakijua ni kosa kisheria.

Ilidaiwa kuwa ujumbe huo ulitumwa kutoka simu namba 0764 150 747 kwenda namba 0766 757 575 uliokuwa ukidai “Karibu, tutakudhibiti kama Uarabuni wanavyodhibiti mashoga.” 


Baada ya kuwasomea maelezo hayo ya awali, washtakiwa hao kwa pamoja walikiri kuwa ni wakazi wa Arusha na Lema ni Mbunge wa
Arusha Mjini ila walikana kusambaza ujumbe huo wa kumtukana Gambo na tarehe ya kukamatwa kwao.Nipashe
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: