BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Wananchi wengi mbumbumbu wa namba za dharura za Zimamoto, Polisi


Licha ya baadhi ya watu kulalamika mara kwa mara kuwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji huchelewa kufika katika maeneo ya ajali za moto, utafiti mpya wa shirika lisilo la kiserikali la Twaweza umebainisha kuwa takriban wananchi wote hawazijui namba za simu za dharura za jeshi hilo.

Matokeo ya utafiti (http://twaweza.or.tz/uploads/files/SzW-Security2017-EN-FINAL-web.pdf) huo uliozinduliwa leo, Alhamisi Julai 27, 2017 yanaeleza kuwa watu 96 kati ya 100 waliohojiwa katika utafiti huo hawazijui namba za jeshi hilo ambazo zingewasaidia kupiga iwapo wamepatwa na ajali ya moto.

Ni mtu mmoja tu kati ya 100 ambao wanajua namba hizo huku wawili kati ya 100 “wanafikiri wanazifahamu lakini hawazifahamu.”

Namba za dharura zinazotumika na Zimamoto nchini ni 114. Kwa mujibu wa tovuti ya jeshi hilo, mwananchi yeyote atakayekumbwa na ajali ya moto au maafa anaweza kupiga wakati wote kwa Saa 24.

Mbali na wananchi kutofahamu namba za Zimamoto, utafiti huo ambao ni mfululizo wa machapisho ya Sauti za Wananchi, unaeleza kuwa bado wananchi wengi hawazijui namba za dharura za polisi jambo linaloweza kuchelewesha kuripoti na kudhibiti matukio ya uhalifu.

“Ni asilimia 4 pekee wanaofahamu namba za simu za polisi, na asilimia moja tu wanaofahamu namba za zima moto. Wengine walifikiri wanafahamu namba hizo, lakini walipoombwa wazitaje, walizikosea,” inasomeka sehemu ya utafiti huo unaoitwa “Hapa Usalama tu: Usalama, polisi na haki nchini”.

Namba za dharura za polisi kwa ajili ya kupiga na ujumbe mfupi yaani SMS ni 111 na 112. 


Kiwango kidogo cha ufahamu wa namba za dharura za majeshi kinapunguza ufanisi wa kukabiliana na majanga na uhalifu nchini kutokana na wananchi kuchelewa kutoa taarifa kwa mamlaka husika ambazo zingewasaidia kwa haraka.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment