BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI ATOA AGIZO KWA VIONGOZI JUU YA WAFANYABIASHARA WA MSAMVU MOROGORO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli 

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amewaagiza viongozi wa Manispaa ya Morogoro na viongozi wa mkoa huo kuwaacha wafanyabiashara ndogondogo waendelee kufanya biashara zao katika eneo la kituo cha mabasi cha Msamvu.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo, Alhamisi 27 Julai 27, baada ya msafara wake uliokuwa ukitoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam kusimamishwa na wananchi wa Morogoro katika eneo la Msamvu na kumueleza kero ya kunyanyaswa na Manispaa ambao wamekuwa wakiwafukuza katika maeneo wanayofanyia biashara hasa baada ya kituo cha mabasi cha Msamvu kujengwa upya.

Rais Magufuli amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, SACP - Ulrich Onesphory Matei kuhakikisha askari mgambo hawawasumbui wafanyabiashara hao na amewataka wafanyabiashara hao kutofanya vurugu wakati utaratibu mzuri unaandaliwa kwa ajili yao.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewataka watu wote waliobinafsishiwa viwanda mbalimbali katika Mkoa wa Morogoro kuvirejesha serikalini endapo wameshindwa kuviendeleza ili wapewe wawekezaji wanaoweza kuviendeleza na kuzalisha ajira.

“Ninarudia wito wangu niliokwisha kuutoa huko nyuma, kwamba wenye viwanda hapa Morogoro ambao wameshindwa kuviendesha, na leo nataja akiwemo Mbunge wa hapa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), narudia akiwemo Mbunge wa hapa wa CCM ambaye alibinafsishiwa viwanda vingi, kama ameshindwa kuviendesha avirudishe ili tuwape watu wengine kwa sababu vijana hawa wanakosa ajira, nazungumza kwa uwazi kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu,” amesisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewapongeza wakulima wa mazao mkoani Morogoro kwa kuongeza uzalishaji wa mazao na amewataja wakulima wa Wilaya ya Kilosa kwa kuongeza uzalishaji kutoka asilimia 42 msimu uliopita hadi kufikia asilimia 82 katika msimu huu.Mwananchi


Kuhusu mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge). 

Rais Magufuli ametoa wito kwa wananchi wa Morogoro kujitokeza kupata ajira wakati wa ujenzi, lakini amewataka waliojenga katika hifadhi ya reli kuondoa majengo yao kwa hiari.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: