BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

FUJO ZALIPUKA BAADA YA UHURU KENYETTA KUTANGAZWA MSHINDI WA URAIS KENYE

Moto GarissaSehemu ya soko kuu mjini Garissa, kaskazini mashariki mwa Kenya, imeteketea baada ya mfarakano kati ya wafuasi wa wagombea wawili wa ugavana katika kaunti hiyo.

Fujo zilizuka baada ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Jumanne kutangazwa.

Ali Bunow Korane wa chama cha Jubilee chake Rais Kenyatta alitangazwa mshindi.

Taarifa zinasema watu wasioridhishwa na matokeo hayo walichoma moto sehemu za soko hilo.

Hali ya utulivu imerejea lakini wazima moto wameendelea kukabiliana na moto huo.

Korane alipata kura 55 335 (51,48%) naye mpinzani wake wa karibu Nathif Jama Adan wa chama cha Wiper akapata kura 50 471 (46,95%), Adan ndiye gavana anayeondoka.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment