BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MGOMBEA MAKAMU WA RAIS TFF, ROBERT SELASELA KUFUMUA MIFUMO MAKUSUDI YA SIMBA NA YANGA.


Mgombea nafasi ya makamu wa rais, Robert Selasema akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) utaonyaika mkoani Dodoma, uzinduzi huo ulifanyika kwenye ofisi za klabu ya waandishi wa habari Morogoro leo, Kshoto ni Mwenyekiti wa klabu hiyo, Nikson Mkilanya. Picha na Juma Mtanda.

Juma mtanda, Morogoro.

Mgombea wa makamu wa rais, Robert Selasela amezindua kampeni ya uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) huku akibainisha mambo manne ikiwemo kuisambaratisha mifumo ya simba na yanga ndani ya shirikisho hilo kwa kuyafanyia kazi endapo tu atashinda katika uchaguzi huo utaofanyika Agosti 12 mjini Dodoma.

Amebainisha mambo hayo kuwa kuwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuinua soka la Tanzania, kusimamia misingi bora ya uongozi ndani ya kamati tendaji, soka la vijana na kusambaratisha mifumo ya klabu ya simba na yanga ndani ya TFF.

Akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa soka mkoani Morogoro, Selesela alisema kuwa ameingia kwa nguvu zote kwenye uchaguzi huo kwa lengo la kutengeneza safu imara ndani ya TFF lakini kuweka mikakati ya kuinua soka la Tanzania na kuondoa mifumo ya usimba na uyanga ili Tanzania iweze kutamba katika soka la ndani na kimataifa.

Katika uchaguzi huo, Selesela atakabiliana na upinzani mkali katika nafasi hiyo kutoka kwa Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani na Stephen Mwakibolwa wanaowania kwa udi na uvumba makamu wa rais wa TFF.

“Nimeingia katika kichang’anyiro cha kugombea nafasi ya makamu wa rais TFF ili kuwa sehemu ya viongozi wataounda timu ya uongozi kwa lengo la kusimamia mikakati ya kuimarisha kwa kuinua soka la Tanzania ikiwemo na kusimamia misingi bora ya uongozi.”alisema Selasela.

Selasela alisema kuwa kuyumba kwa soka la Tanzania kunatokana na usimamizi kutoka ndani ya TFF katika usimamizi wa mifumo yote lakini endapo kutakuwa na safu imara ya kamati tendaji, TFF itasonga mbele kupitia kamati ya mipango ya fedha na mipango.

“Nitakuwa msimamizi mzuri wa Kamati ya mipango na fedha katika safu ambayo mimi nitakuwa ndani ili kusimamia vyema katika matumizi sahihi ya fedha kwani endapo kamati hiyo ikikosa watu makini TFF itayumba na soka letu litaendelea kuyumba mwaka hadi mwaka.”alisema Selasela.”

Aliongeza kwa kusema kuwa kamati hiyo inajukumu kubwa katika kuendeleza soka la vijana, soka la wanawake na timu ya taifa na ili uweze kupata timu iliyo bora lazima kuwe na mipango imara katika soka la vijana na ligi zote zinazosimamiwa na TFF.

Akitolea mfano, Selasela alisema kuwa michuano ya vijana ya copa coca cola imekufa, imebakia mashindano ya Airtel Rising pekee lakini hata ligi ya taifa cup sasa hivi haichezwi huku na kuwa mashindano ngazi ya wilaya ndiko chimbuko la kuibua vipaji vya wachezaji katika soka la Tanzania na mashindano ya vijana.

Katika mkutano huo, Selasela aliweka bayana kusimamia vizuri vyama vya soka vya mikoa na wilaya ambako katika safu hiyo ya uongozi kuhakikisha ligi ngazi ya wilaya linafanyika kutokana na kalenda tofauti na hivi sasa ambako baadhi ya wilaya wameshindwa kuendesha ligi daraja la nne.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment