BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KOREA KASKAZINI YAIONYA MAREKENI

Korea Kaskazini imetupilia mbali pendekezo kutoka Korea Kasuni la kutaka wafanye mazungumzo.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Kang Kyung-wha alikuwa ametoa pendekezo hilo kwa mwenzake wa Korea Kaskazini Ri Yong Hi, pembezoni mwa mkutano wa kikanda siku ya Jumapili huko Manila, Ufilipino.
Mawaziri wa Korea Kaskazini na Kusini wafanya mkutano Manila 

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vilisema kuwa hakutakuwa na mazungumzo kuhusu mpango wake wenye uta wa nuklia wakati inakumbwa na vitisho kutoka Marekani.

Pia ilipinga vikwazo vipya ilivyowekewa na Umoja wa Mataifa siku ya Jumapili

Msukosuko umeshuhudiwa katika rasi ya Korea miezi ya hivi karibuni huku majaribio kadha ya makombora yakifanywa na Korea Kaskazini.

Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa siku ya Jumapili lilipiga kura kuwekea Korea Kaskazni vikwazo zaidi.

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini viliripoti kuwa Bi Kang alisalimiana kwa mkono na bwana Ri wakati wa mkutano uliokuwa mfupi ulioandaliwa na nchi za Asean.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: