BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Lissu bado anashikiliwa na Polisi

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu

Dar es Salaam.
Wakili Frederick Kihwelo amesema mteja wake Tundu Lissu ameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kati hadi muda huu( 5:50) na hakuna dalili za kufikishwa mahakamani kama walivyokubaliana jana.

Kihwelo ameliambia gazeti hili kwamba, jana maofisa wa Polisi walimuhakikishia kwamba leo angefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma zinazomkabili.

Jana, mawakili wa mbunge huyo wa Singida Mashariki walishindwa kufanikisha dhamana na alilala rumande huku polisi wakitumia saa moja na nusu kumpekua Lissu nyumbani kwake,wakitafuta nyaraka zinazohusiana na kushikiliwa kwa ndege hiyo.

"Bado tunaendelea kufuatilia lakini ikifika mchana,kuanzia saa 8:00 tutachukua hatua nyingine kama hawatakuwa wamemfikisha mahakamani, leo tumefika mahakamani asubuhi tukijua watamleta huku(Kisutu) kama tulivyokubaliana lakini hakuna dalili,"amesema Kihwelo.

"Hatujafahamu nini kilichosababisha wasimfikishe hadi sasa.tutawasiliana baadaye kwa hatua zaidi, tunaweza kuiomba mahakama iwaamuru wamfikishe mahakamani."

Lissu alikamatwa juzi jijini Dar es Salaam, akiwa maeneo ya mahakama hiyo ya Kisutu, akituhumiwa kwa madai ya kumkashifu rais wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea siku chache zilizopita. 


Siku ya mkutano huo, Lissu aliibua sakata linalohusu Kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd(SCEL), kuishikilia Ndege ya Bombardier Dash 8 nchini Kanada,hadi itakapolipwa deni lake la Sh87bilioni.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: