BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAHASIDI WALIOKULA NJAMA YA KUUA WAZAZI WAO KWA TAMAA YA MIRATHI MALI



Na Geofrey Chambua.
Huenda unajutia mtoto wako ni mtukutu bila kujua kwamba wapo watukutu wasio mfano

Mwaka 1989 ndugu wawili wajulikanao kama Lyle ambaye kwa sasa ana miaka 49, na Erik ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 46, waliowaua wazazi wao kwa kuwapiga risasi sehemu mbalimbali za miili yao.

Mauaji hayo yalitokea katika jumba lao la kifahari lililokuwa Beverly Hills, na kipindi hicho Lyle alikuwa na umri wa miaka 21 na Erik miaka 18.

Lyle ndiye aliyepiga simu ya dharura 911 kutoa taarifa kuwa wamerudi nyumbani na kukuta wazazi wao wameuawa.

Siku hiyo ilikuwa siku ya Jumapili ya mwezi wa nane mwaka 1989.
Baada ya polisi kufika eneo la tukio walikuta maiti mbili za watu maarufu waliokuwa wakijulikana kwa kila mtu, yani Bwana Jose na Mkewe Bi Kitty.

Polisi hawakuwa na wazo kabisa kuwa mauaji hayo yanaweza kuwa yamefanywa na vijana hao hivyo walibaki wakiowaonea huruma kwa kufiwa na wazazi wao.

FAMILIA YA LYLE NA ERIK

Lyle na Erik walizaliwa katika familia ya kitajiri yenye ukwasi wa kutosha. Baba yao Jose alikuwa kati ya wakurugenzi wa juu kabisa Hollywood, huku mama yao Kitty aliwahi kuwa mshindi wa taji la urembo, ambaye kwa muda huo alikuwa akijishughulisha na upambaji wa makazi pamoja na shughuli za kusaidia jamii.

Baba yao yani Jose, inasemekana alikuwa mkali sana, asiyependa masikhara hata kidogo linapokuja suala la masomo.

Pia inasemekana alikuwa na matumaini makubwa sana juu ya watoto wake akiwa anategemea waje kuwa watu wakubwa na maarufu huko mbeleni.


Lakini Lyle na Erik mara zote walishindwa timiza ndoto ya baba yao kwa kutofaulu vizuri katika masomo yao, pia walijihusisha na makundi ya wavuta bangi na madawa ya kulevya huku wakiwa wadokozi kwenye majumba ya watu jambo ambalo liliwakosesha amani baba na mama yao.

NINI LILITOKEA 20/08/1989
Lyle na Erik waliwatwanga risasi wazazi wao wakiwa sebuleni, kisha wakatengeneza mazingira yaonekane kama vile lilikuwa tukio la uvamizi.

Baada ya hapo waliondoka nyumbani wakiacha maiti za wazazi wao, wakaelekea kwenye sinema wakanunua tiketi ya kuangalia movie ili kutengeneza ushahidi kuwa hawakuwepo wakati wazazi wao wakiuawa.

Baada ya movie walikutana na marafiki wakazurura nao mpaka usiku wa manane ndipo waliporejea nyumbani kwao.

Lyle alipiga simu 911 akipiga kelele na kulia kuwa wazazi wao wameuwa.
Polisi walipofika waliwakuta wakiwa wanalia na kupiga kelele jambo lililowatia simanzi na hawakuwashuku kabisa kama wao ndiyo wauwaji.

Na ajabu ni kwamba bunduki walizotumia kuwaua wazazi wao walikuwa bado wanazo kwenye gari lao lakini polisi hata hawakulipekua.

SIRI YAFICHUKA

Baada ya mauaji hayo vijana hao ndiyo walibaki kama warithi wa mali za wazazi wao, nao bila kuchelewa walianza kuzotumbua kwa kununua magari ya kifahari na vito vya thamani.

Yale majonzi waliyoyaonuesha siku ya tukio yalipotea ghafla wakaanza kula maisha.

Inasemekana ndani ya mwezi mmoja walikuwa wametumia kiasi cha dola 500,000-700,000.

Tabia yao ya kutumbua pesa iliawashtua polisi na kuwafanya waanze kuwachunguza.

Kwa upande mwingine Erik alisumbuliwa sana na tukio walilofanya yeye na kaka yake, akawa anatafuta mtu wa kumwambia, na ndipo akaamua amwambie rafiki yake aitwaye Craig.

Hakuishia hapo alimfuata mwanasaikolojia aitwaye Jerome na kukiri juu ya mauaji hayo.

Lyle alipojua kuwa Erik kakiri kwa mwanasaikolojia alimfuata Erik akamaambia waongozane kwa huyo mwanasaikolojia, na wote walikiri mbele yake ila Lyle akamtishia kuwa akisema tu atamuua.

Lyle alikubali kuwa yeye ndiye alimpiga risasi ya kichwa baba yake na mkono mama yake na mdogo wake akammalizia mama yake kwa kumpiga risasi nyingine mpili na kumfumua kichwa.

Pia anadai sababu ni kwamba walikuwa wakiishi kwa hofu ya kuwa baba yao atawaua kwakuwa alikuwa akiwapiga na kuwatesa hata kuwaingilia kinyume na maumbile, hivyo alijua ipo siku watakuja sema kwa hiyo angewaua kabla ya wao kutoa siri.

Kuhusu mama yao anadai alijua yote waliyokuwa wanafanyiwa na baba yao lakini hakufanya lolote kuwasaidia.

Pia anasema ana amani kuwa gerezani kwakuwa ndiko anadhani anastahili kuwa kwa kuwaua wazazi wake.

Wakati akiendelea na simulizi ya picha ya tukio, kumbe muda huo alikuwepo kimada wa Jerome maeneo ya ofisini hivyo wakato yuko nje ya ofisi alisikia mazungumzo yao na akawarekodi.

Huo ushahidi alibaki nao wala hakuupeleka polisi mpaka baada ya miezi saba aliposikia kuwa wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuwaua wazazi wao ndipo naye akapeleka ushahidi.

Wote walifungwa vifungo vya maisha magereZa tofauti na toka kipindi hicho hawajahi kukutana zaidi ya kuandikiana barua.

Na wote wamefanikiwa kuoa wakiwa gerezani......KWA WENZETU Unaruhusiwa kuoa ukiwa gerezani. Pia inatokana na kosa la mfungwa,kuna kitu kinaitwa "Conjugal Visit" hii inampa mfungwa haki ya kukutana na mume au mke wa ndoa katika sehemu maalum gerezani na kufanya tendo la ndoa kwa masaa kadhaa au hata siku mbili au tatu (inatokana na tabia ya mfungwa akiwa anatumikia kifungo gerezani).
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: