BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MARUBANI WAFUKUZWA KAZI BAADA YA KUMRUHUSU MTOTO YATIMA KUENDESHA NDEGE YA SERIKALI

Marubani wawili wanaofanya kazi na shirika la ndege la serikali nchini Algeria wamefukuzwa kazi baada ya kumruhusu mtoto yatima mwenye umri wa miaka kumi kuendesha ndege ya abiria.

Mtandao wa Africa News unasema kuwa zoezi hilo liifadhiliwa na kurekodiwa na runinga ya El Bilad TV, waliomuonyesha mtoto huyo akiwa amavaa sare za rubani akibofya vitufe katika chumba cha rubani.

Haijulikani ni abiria wangapi walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Air Algerie kutoka mji wa Algiers hadi mji Setif.

Mtandao huo unasema kuwa rubani hao walifukuzwa tarehe 29 mwezi Julai huku uchunguzi zaidi ukifanywa kwa sababu kitendo hicho kilikiuka sheria za usafiri wa ndege.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: