
Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar (25) ameruhusiwa kuzungumza rasmi kuhusu uhamisho wake wa rekodi ya dunia wa pauni milioni 198 kwenda Paris St-Germain.
Mchezaji huyu wa kimataifa wa Brazil amewaambia wachezaji wenzake siku ya Jumatano kuwa anataka kuondoka Barcelona.
Amepewa ruhusa na meneja wake Ernesto Valverde ya kutokwenda mazoezini na “kutatua hatma yake”.
Mkataba wa Neymar una kifungu cha euro milioni 222 ambacho PSG wapo tayari kukitengua ili kuweza kukamilisha usajili.

0 comments:
Post a Comment