BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTANZANIA AWEKA REKODI MBIO NDEFU ZA MARATHON NCHINI UINGEREZA

Mwanariadha Alphonce Simbu ameshinda medali ya shaba katika mbio ndefu za Marathon akimaliza nafasi ya tatu katika Mashindano ya Dunia ya Riadha London, Uingereza.

Simbu alikimbia kwa saa 2:09:51 na kumaliza kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Mkenya, Geoffrey Kirui aliyemaliza kwenye nafasi ya kwanza akikimbia kwa saa 2:08:27 na Muethiopia, Tamirat Tola aliyemaliza wa pili akikimbia kwa saa 2:09:49.

Ushindi huo wa Simbu ni neema kwa Tanzania ambayo tangu 2005 ilipochukua medali kwenye mbio hizo huko Finland, haijawahi kushinda medali yoyote ya dunia hadi leo Jumapili Simbu kushinda Shaba.

Medali hiyo ya Simbu ilianza kuonekana mapema wakiwa wamekimbia umbali wa kilomita 21 (Nusu Marathon).

Kwa ushindi huo sasa Simbu ataondoka na kitita cha Dola 20,000 huku bingwa akizawadiwa Dola 60,000 na mshindi wa pili ataondoka na Dola 30,000.

Mwanariadha Alphonce Simbu ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza tangu mwaka 2005 kunyakua medali ya Shaba kwa kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Riadha ya Dunia yanayofanyika nchini Uingereza/http://www.mwanaspoti.co.tz
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment