BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDEGE YA ABIRIA YA UFARANSA NUSURA IPIGWE NA KOMBORA LA MAJARIBIO LA KOREA KASKAZINI IKIWA NA WATU 330


Ndege moja ya Ufaransa iliokuwa na abiria 330 ilikuwa kilomita 100 pekee na kombora la masafa marefu lililorushwa na Korea Kaskazini maafia wanasema.

Ndege hiyo ilipita katika eneo ambalo kombora hilo lilinguka dakika 10 baadaye.

Kampuni ya Airfrance inasema kuwa ndege yake haikuwa hatarini lakini imejiweke marufuku ya kusafiri katika anga ya Korea Kaskazini kama tahadhari.
Pentagon inasema kuwa kombora hilo lilipaa katika anga yenye shughuli nyingi.

Maafisa wa Marekani nara kwa mara wamekuwa wakionya kuhusu hatari zinazoletwa na makombora dhidi ya ndege za abiria katika eneo hilo. Kombora la masafa marefu ICBM

Njia iliotumiwa na ndege hiyo aina ya Boeing 777 inaonyesha kuwa ilikuwa magharibi, mwa Hokkaido, kaskazini mwa taifa la Japan , wakati bora hilo la Korea Kaskazini lilikuwa hewani.

Japan na Marekani inakadiria kwamba kombora hilo lilianguaka kati ya kilomita 100na 150 karibu na ndege hiyo.

"Kombora hilo liliruka katika anga na kuanguka nchini Japan, eneo ambalo hutumika na vyombo vya kibiashara na vile vya uvuvi , msemaji wa Pentagon Jeff Davis alisema
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: