BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI AWATOLEA NJE WANAOTAKA KUONGEZEWA MUDA WA KUONGOZA TANZANIA

 
Rais John Magufuli amesema hawezi kukaa madarakani kwa miaka 20 kwa kuwa anaheshimu Katiba na kwamba kazi ya urais ni ngumu.

Magufuli amesema hayo leo Jumatatu, Agosti 7 katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga alipozungumza na wananchi na kuzindua stendi ya kisasa ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya siku tano mkoani Tanga.

Kauli hiyo ya Rais imekuja baada ya Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani kusema kwa kuwa Magufuli anafanya kazi nzuri itakuwa vizuri akiongezewa hata miaka 20. 


“Nadhani Profesa Maji Marefu unataka niishi miaka 20 zaidi na siyo kuwa rais kwa miaka 20 kwa kuwa sitafanya hivyo kwa kuwa naheshimu Katiba,” alisema.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: