BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ROBERT SELASELA, KATIBU TAWALA ANAYEGOMBEA NAFASI YA MAKAMU WA RAIS TFF

Robert Selasela ni Katibu Tawala wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro aliyejitosa kugombea nafasi ya makamu wa rais katika uchaguzi mkuu wa TFF.

Juma mtanda, Morogoro.

Robert Selasela ni Katibu Tawala wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro ambaye amejitosa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya makamau wa rais ndani ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu utaofanyika Dodoma.

Amejitosa na kuanika mipango yake na kuwa ana jukumu maalumu la kusimamia kabumbu kupitia kamati mama ya mipango na fedha ndani ya TFF kwa kudokeza kuwa bila kamati hiyo ya fedha hakuna soka na bila fedha hakuna maendeleo ya soka.

Akizungumza na MTANDA BLOG, Selasela alieleza kuwa anaomba ridhaa ya wajumbe ili kusaidiana na viongozi wataochaguliwa ili kurudisha mpira katika mikono salama ili mpira usonge mbele na kurudisha enzi za Mogela, Sembuli na wengine waliong’arisha Tanzania.


Tunataka kuifanya Tanzania kuwa mashujaa na mimi falsa yangu ni soka bora fulsa ya ajira na hii inawezekana kama wajumbe watanichagua kwenye nafasi ya makamu wa rais ili kushirikiana na uongozi mpya ili soka lichezwe bila ubabaishaji.Alisema Selasela.

Selasela ambaye amekuwa Mwenyekiti wa chama cha soka Morogoro Vijijini, Diwani kata ya Kiroka na kiongozi wa timu mbalimbali ameeleza kuwa moyo wa TFF upo katika kamati ya mipango na fedha na soka ndio mchezo wenye nguvu zaidi dunia na unaopendwa na watu wengi.

“Nina uwezo mkubwa wa kuwa kiongozi ndani ya TFF na nitaongoza vyema kamati ya mipango na fedha kama makamu wa rais na hii ndio roho ya TFF kwani mipango yote inaanzisha katika fedha na inamhitaji Selasela atayeshirikiana na wenzake kuunda uongozi imara.”alisema Selasela.

Selasela ameeleza kuwa kamati ya mipango na fedha ikikaa vizuri vyama vya soka vya mikoa na wilaya vitakaa vizuri kwani vimekuwa vikishindwa kusimamia soka kutokana na kutowezeshwa kiongozi, kifedha hata kusimamiwa kwa maslahi ya maendeleo ya soka la Tanzania.

Nitakuwa sehemu ya kujenga mifumo bora ya utawala ndani ya TFF kwa kutengeneza nidhamu kuanzia matumizi ya fedha, uongozi ndani ya shirikisho hilo na vilabu vyote vya ligi kuu, daraja la kwanza na ngazi ya mkoa na wilaya kwani mifumo iliyopo ni mibovu na inahitaji kufumuliwa.

Mifumo ya utawala ndani ya TFF haujakaa vizuri kutokana na malalamiko kibao ya tuhuma za rushwa kwa viongozi lakini hata suala la upangaji matokeo hivyo inahitaji viongozi wenye udhubutu wa kuondoa mifumo hiyo na kutengeneza nidhamu ili TFF iwe chombo safi.alisema Selasela.

TFF ikikaa vizuri itaweza kusaidia serikali katika upatikanaji wa ajira rasmi kupitia mchezo wa soka katika ngazi ya ligi kuu hadi madaraja ya chini ambako kuna vijana wengi na wengine wamekuwa wakijiingiza katika katika vitendo vya uhalifu kutokana na kujiondoa kwenye soka kutokana na usimamizi mbovu.

“Siendi TFF kutafuta kazi bali ninaenda kuomba nafasi ya uongozi na hii maana yake kuwa wenye lengo la kutafuta kazi TFF, hawana lengo la kuongoza mpira bali wanatafuta kazi na matokeo yake, kile kinachoingia TFF kimekuwa hakiendi katika maendeleo ya soka.”alieleza Selasela.

Selasela aliongeza kwa kueleza kuwa serikali imesisitiza watu kufanya kazi lakini kupitia soka, viongozi wanaweza kutengeneza ajira na kupunguza wimbi la vijana kujiingiza kwenye uhalifu.

Kama nikishinda nitaongea na rais wa TFF kukusanya ilani zote za wagombea na kutengeneza kitu kimoja yenye dira ya pamoja ya kukusanya mawazo na kuyafanyia kazi katika uendeshaji wa mpira wa Tanzania.aliongeza.

Viongozi wanaswa kuwa na utayari wa kutumikia mchezo wa soka kwa kuweka mikakati dhabiti ya kuinua soka la Tanzania, kusimamia misingi bora ya uongozi, soka la vijana na wanawake katika kuangalizia vipaji ngazi ya shule za msingi na usimamizi wa ligi zote bila kujali timu.

TFF lazima iwe chachu ya maendelea ya soka endapo tu itaweka misingi bora, leo hii yapo wapi mashindano ya vijana ya Copa coca cola na Airtel Rising Stars ni kama inayumba lakini yapo wapi mashindano ya taifa Cup ?.

AWAOMBA WAJUMBE.
Uchaguzi wa kupangapanga watu hautaweza kupata viongozi wataotumikia vyema soka, bali kutapatikana viongozi wasio sahihi na badala yake soka la Tanzania litaendelea kudidia siku hadi siku ni lazima kupata viongozi wenye kuinua soka.

Selasela amewaomba wagombea wenzake katika nafasi ya makamu ya rais na wajumbe wa mkutano mkuu kumpigia kura ya ndio ili aweze kushinda nafasi ya makamu wa makamu kwa kuamini kuwa yeye atakuwa chaguo sahihi kutokana na kuwa na uwezo wa kuongoza.

Alidai kuwa kuyumba kwa soka la Tanzania katika mashindano ya kimataifa kumetokana na usimamizi mbovu hasa katika matumizi bora ya fedha katika shirikisho la soka Tanzania.

Naenda kusimamia kamati nyeti ya fedha, mpira ni fedha na mimi naenda kufanya kazi ya kusimamia kamati ya mipango na fedha kupitia nafasi ya makamu wa rais na kamati yangu ndio roho ya mpira.

Utawala bora ni kama hesabu na utawala bora unagusa kila sehemu na ukiwa na viongozi wa vilabu vyetu ambao sio viongozi bora kutakuwa na timu iliyokosa nidhamu kuanzia viongozi hadi wachezaji hivyo lazima kuwe na mipango ya kutengeneza safu ya viongozi bora katika familia ya soka.alisema Selasela.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment