BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU 11 WAUAWAWA NA POLISI WAKATI WA MAANDAMANO.

Taarifa kutoka Kenya zinasema jumla ya watu 11 wameuawa na polisi katika mji wa magharibi wa Kisumu na baadhi ya maeneo ya mabanda jijini Nairobi katika jitihada za kukabiliana na maandamano yaliyosababishwa na tangazo la kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru Kenyatta.

Miili ya vijana 9 waliouawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo katika eneo la Mathare jijini Nairobi imepelekwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti, afisa mmoja wa usalama ameliambia shirika la habari la Reuters. 

Mbali na hao, msichana mdogo aliuawa baada ya polisi kufyatua risasi kwa nyakati tofauti, kwa mujibu wa shuhuda. Kitongoji hicho ni ngome ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga mwenye miaka 74 ambaye chama chake kilikataa matokeo ya awali na kusema kulikuwa na udanganyifu.

Vurugu hizo zimezuka baada ya tume ya uchaguzi na mipaka IEBC, kumtangaza Kenyatta usiku wa jana Ijumaa kuwa amechaguliwa tena kwa kipindi cha miaka mitano, licha ya madai ya upinzani kwamba zoezi la kuhesabu kura lilikuwa na kasoro.

Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i amesema vurugu zimethibitiwa na kwamba kuna dalili za uhalifu lakini sio maandamano ya kisiasa.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment