BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UGONJWA: MBUNGE WA BUNDA MJINI ESTER BULAYA HAWEZI KULA MWENYEWE WALA KUOGA BAADA YA KULAZWA KWA MARADHI HOSPITALINI


Wakati Mbunge wa Bunda mjini, Ester Bulaya akiendelea kusaidiwa kuogeshwa na kulishwa wodini kutokana na kutojimudu, viongozi wa Chadema wanaomuuguza wameelezea kuridhishwa na hali yake,

Mbunge huyo ameanza kujitambua tangu alipofika hospitalini baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya Kituo cha Kati cha Polisi mjini Tarime.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Tarime, Lucas Ngoto ameieleza Mwananchi asubuhi hii Agosti 21 kuwa mbunge huyo ameanza kujitambua, kuzungumza na kula chakula kidogo kwa kulishwa tofauti na jana alipokuwa hajitambui.

Mgoto amesema uongozi wa Chadema kupitia kwa Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko unaendelea kufanya jitihada za kuwasiliana na uongozi wa jeshi la polisi ili mbunge huyo apewe dhamana kumwezesha kwenda jijini Dar es Salaam kuonana na daktari wake anayemtibu kuhusiana na tatizo lake la njia ya hewa inayomsumbua kwa muda mrefu.

Bulaya amesota rumande tangu akamatwe Ijumaa ya Agosti 18 kwa madai ya kuingia jimbo la Tarime na kufanya shughuli za kisiasa kwa kutoa msaada wa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi jimboni humo baada ya kualikwa na mbunge mwenzake Ester Matiko.

Wakati Bulaya akikamatwa na kusota mahabusu kwa kushiriki shughuli za maendeleo na kusalimia ananchi kkwenye jimbo la uchaguzi lisilo lake, matukio ya wabunge wa majjimbo kuwaalika wenzao kusaidia juhudi za mmaendeleo na kusalimia wananchi katiika mikutano ya hadhara yameshuhudiwa sehemu mballimbali nchini bila kuingiliwa na polisi.

Miezi miwili iliyopita mbunge wa jjimbo la Msalala, Ezekiel Maige aliwaalike wenzake Joseph Kasheku "Msukuma” na Selemani Zedi jimboni kwake ambapo walihudhuria mkutano wa hadhara na kuhutubia wananchi.

Siku chache ziilizopita mbunge wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe alimwalika Goodbless Lemaa wa Arusha mjini katika mkuutano wake wa hadhara jimboni kwake bila ambapo alihutubia mkutano wa hadhara bila kuwepo mkwaruzano kati ya vioƱgozi hao na polisi.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: