BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WALLACE KARIA AMMBWAGA ALLY MAYAI NAFASI YA URAIS TFF MJINI DODOMA

Wallace Karia amewabwaga wapinzani wake na kuwa Rais mpya wa TFF akiwemo Ally Mayai aliyekuwa anapewa nafasi ya kushinda kiti hicho katika uchaguzi mkuu uliofanyika mjini Dodoma leo.
 

Karia ameibuka na kura 99 baada ya wajumbe kumpigia kura za ndio huku wapinzani wake wakipata wastani wa chini ya kura 10.

Karia ambaye uongozi ulioisha muda wake alikuwa na wasfa wa Kaimu Rais wa TFF, ametwaa nafasi hiyo baada ya mchuano mkali katika uchaguzi mkuu huo.


Katika matokeo hayo ya mgombea Emmanuel Kimbe alipata kura moja, Mwakalebela akipata kura tatu, Madega kura nane, Shija Richard kura tisa, Ally Mayay kura tisa na Wallace Karia akizoa kura 95.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment