BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKLALI YA KENYA YACHIMBA MKWALA NZITO KWA KUKABILIANA NA WAANDAMANAJI WAHALIFU


Kaimu waziri wa usalama nchini Kenya Fred Matiangi


Kaimu waziri wa usalama nchini Kenya Fred Matiangi amesema kuwa polisi hawatasita kulinda maisha ya Wakenya na mali yao kufuatia kukamilika kwa uchaguzi uliokumbwa na utata.

Rais Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi na hivyobasi kuhifadhi kiti chake.

Matiangi alikosoa utumiaji mbaya wa mitandao ya kijamii na kusema baadhi ya raia wamekamatwa.

Amesema kuwa kumekuwa na ghasia katika sehemu chache ambazo amelaumu kutekelezwa na wahalifu.

Upinzani unasema kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa ikiwemo watoto kumi ijapokuwa haujatoa ushahidi wowote wa madai hayo.

Umesisitiza kuwa hautakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment