BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

GAZETI LA MwanaHALISI LAFUNGIWA MIAKA MIWILI KWA KUANDIKA HABARI ZA UONGO NA UCHOCHEZI

Serikali ya Tanzania imelifungia gazeti la Mwanahalisi kwa miaka miwili zuio hilo pia linahusisha machapisho ya mtandaoni.

Gazeti hilo linafungiwa kwa kile kilicho arifiwa kuwa ni kuchapisha habari za uongo na uchochezi ambazo zinadaiwa kuwa zinaweza kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

Mwanahalisi linakuwa gazeti la pili kufungiwa kwa kipindi cha miezi minne.

Gazeti hilo limepigwa kufuli kutokana na kuchapisha mlolongo wa habari ambazo zinasemekana kuwa za kichochezi ikiwemo yenye kichwa cha habari 'Tumwombee Magufuli au Tundu Lissu' iliyochapishwa katika toleo la 409 la tarehe 18-24 Septemba 2017 .

Hivi karibuni vyombo vya habari vimekuwa vikimulikwa kwa ukaribu nchini humo. Mapema mwaka huu Raisi Magufuli alionya vyombo vya habari 'visifikiri viko huru kwa kiwango hicho.'
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: