
Kituo cha Magic FM kilicho mjini Dar Es Salaam na kile cha Radio Five ambacho kinapepeperusha matangazo yake kutoka mjini Arusha vitafanyiwa uchunguzi na wizara ya habari.
Hatua hii inakuja wiki chache baada ya serikali kulifunga gazeti la Mseto kwa kuchapisha habari zisizo za ukweli.
Rais Magufuli alipiga maruguku mikutano yote ya kisiasa wakati aliingia madarakani mwaka uliopita, lakini chama cha upinzani cha Chadema kinasema kuwa kina mipango ya kuendelea na mikikutano hiyo.
Chadema kinapinga sheria dhidi ya ulalifu wa mitandao kikisema kuwa zinaingilia kati uhuru wa kujieleza
0 comments:
Post a Comment