BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATOTO WA WAFUGAJI WATUHUMIWA KUANZISHA MAPIGANO MVOMERO

Juma Mtanda, Morogoro.
Siri ya kushamiri kwa migogoro inayopelekea mapigano kati ya wafugaji na wakulima imetajwa kusababishwa na watoto wanaopewa kazi ya kuchunga makundi makubwa ya mifugo huku wakidaiwa kushindwa kuimudu kutokana na kuwa na akili yenye upeo mdogo inayopelekea mifugo kuingia kwenye mashamba yenye mazao katika vijiji vingi vya wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Wakizungumza wakati wa mdahalo uliowakutanisha wakulima na wafugaji kijiji cha Dakawa wilayani humo walisema kuwa moja ya vyanzo vya migogoro inayopelekea mapigano ni wafugaji kukabidhi watoto kundi la mifugo kwenda kuchunga huku wakitambua wana upeo mdogo wa uwelewa.

Mdahalo huo una lengo la kudumisha amani na kusuluhisha migogoro ulioandaliwa na shirika la Tanzania Initiave For Social Economic Relief (Tiser) kupitia mradi wa kuhimiza matumizi bora ya ardhi yenye tija na utawala bora wa ushirikishwaji wadau katika kutengeneza sera bora.

Fahamia Ally alisema kuwa kuwa visa vingi vinavyozalisha migogoro na kupelekea mapigano kati ya wakulima na wafugaji vinasabishwa na watoto wenye umri kati ya miaka mitano hadi 10 ambao hupewa kundi kubwa la mifugo na kushindwa kuimudu hasa maeneo ya jirani na mashamba.

Fahamia alidai kuwa watoto hao wamekuwa wakitumia fimbo na sime kama njia ya kujitetea pindi wanapoingiza mifugo shambani ama kwa bahati mbaya au makusudi na wako tayari kukudhuru kwa kukushambulia na silaha hizo.

“Wakati sasa umefika kwa wafugaji kubadilika wanapaswa kuwapelekea watoto shule na kazi ya kuchunga mifugo ifanywe na watu wazima kwani migogoro inayopelekea machafuko inachangiwa na watoto kutokana na upeo wao mdogo wa akili wa kuchambua baya na zuri.”alisema Fahamia.

Luenda Kibaila anayefuga na kulima alisema kuwa migogoro kati ya wafugaji na wakulima wakati mwingine imekuwa ikichangiwa na wafugaji wasio na makazi maalumu pindi wanalisha mifugo shambani hushikwa mifugo ya wenyeji.

Kibaila alisema kuwa wafugaji wenyeji wamekuwa wakiishi vizuri na wakulima na hata inapotokea mifugo imeingia kwa bahati mbaya shamani hukaa pamoja na kumaliza kwa njia ya amani.

Afisa mtendaji wa kijiji cha Dakawa wilaya hiyo ya Mvomero, Andrew Mohamed alisema kuwa changamoto kubwa inayowakuta viongozi wa kijiji kukosekana kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi na muingiliano wa mipaka.

“Kuna wakati viongozi tumekuwa tukihaha kusuluhisha migogoro na migogorom mingi ndani ya kijiji hiki inamalizwa kwa njia ya amani lakini tuna changamoto ya mpango wa matumizi bora ya ardhi na mipaka kutotambulika inayopelekea kuwa na mifugo mingi.”alisema Mohamed.

Shirika la Tanzania Initiave For Social Economic Relief (Tiser) limekuwa likikusanya maoni kwa kutumia njia ya kudumisha amani na kusuluhisha migogoro kwa wakulima na wafugaji katika wilaya ya Mvomero kupitia mradi wa kuhimiza matumizi bora ya ardhi yenye tija na utawala bora wa ushirikishwaji wadau katika kutengeneza sera bora.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: