BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWIGULU NCHIMBA ASHIRIKI UJENZI NYUMBA ZA POLISI ARUSHA

Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba akishiriki ujenzi wa nyumba za Polisi Arusha kwa kuweka tofali na saruji mara baada ya kufanya ukaguzi na kupata maelezo juu ya maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo.

Na Rashid Nchimbi, Polisi Arusha.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba leo Mchana ametembelea jijini Arusha na kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba za Polisi zinazoendelea kujengwa baada ya ajali ya moto iliyotokea mwishoni mwa mwezi Septemba ambayo ilisababisha familia za askari 13 kuunguliwa vitu mbalimbali na kukosa makazi.

Mh. Mwigulu alitumia fursa hiyo kwa kuishukuru kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ambayo inaoongozwa na Mkuu wa mkoa Mh. Mrisho Gambo lakini pia aliwashukuru wadau ambao wote kwa pamoja walichukua hatua za haraka za kurejesha makazi ya askari ambao walikumbwa na janga la moto huku akisisitiza kwa kusema kwamba hali ilioonyeshwa na wadau hao ni mfano mzuri wa kuigwa na mikoa mingine waone nchi inajengwa na wananchi.

Alisema kwamba suala la makazi ya askari lipo katika kipaumbele cha serikali na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameonyesha kwa vitendo katika maeneo tofauti ikiwemo hapa Arusha.

Alisema Serikali ikishamaliza hilo itaendelea na utaratibu mwingine wa kujenga majengo ya kisasa ili askari wapate makazi bora huku akimuagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha awafikishie salamu askari wa Arusha kwamba, Mh. Rais yupo pamoja nao na Wizara ipo pamoja nao.
 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo mbali na kuendelea kuwashukuru wadau hao kwa kujitolea na kumuunga mkono Rais ambaye alionyesha njia siku hiyo hiyo usiku kabla hakujapambazuka kwa kutoa mchango wake kama Serikali, lakini pia alisema bado milango ipo wazi kwa watu wengine ambao hawakuwa na taarifa juu ya tukio hilo ili kulisaidia Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha liweze kufanikisha ujenzi wa makazi ya askari hao.

Kamanda Mkumbo aliongeza kwa kusema ujenzi wa makazi bora ya askari mkoani hapa utasaidia kuwaongezea morali zaidi wa kazi askari hao hali ambayo itazidi kuimarisha usalama na shughuli za maendeleo kusonga mbele.

Jumla ya nyumba 29 za askari katika moja ya kambi iliyoathirika na ajali ya moto zilianzwa kujengwa toka tarehe 2 mwezi huu jijini hapa na saba ambazo zipo katika ngazi ya msingi zinatarajiwa kujengwa katika kituo kidogo cha Polisi Morombo kata ya Murieti.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: