BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS TEODORO NGUEMA, KIONGOZI ASIYE NA CHEMBE YA HURUMA KWA WATU ANAOWAONGOZA

JINA la Teodoro Obiang Nguema linaweza lisijulikane sana duniani, lakini kwa wananchi wa Equatorial Guinea, nchi ndogo iliyoko magharibi mwa Afrika, huyo ni kiongozi dhalimu na katili asiye na huruma kabisa na watu wake, na wapinzani wake wanadai kuwa hukata, hupika na kutafuta kende na ubongo wa wapinzani wake baada ya kuwa amewaua.

Teodoro Obiang Nguema mwenye umri wa miaka 74 na ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1979 hutafuta kende na ubongo wa wapinzani wake kwa madai kuwa sehemu hizo za miili ya binadamu zinamwongezea nguvu za kiume.

Nguema ambaye ni kiongozi wa pili katika Afrika, nyuma ya Paul Biya wa Cameroun kuendelea kukaa madarakani kwa muda mrefu zaidi katika Equatorial Guinea, hujulikana, na hasa miongoni mwa wapinzani wake kama “kamanda wa utesaji wa watu”. Kwa wale waliofanikiwa kunusurika kutoka utawala wake wa mauaji wanamwona kiongozi huyo kama “uovu wenyewe”.

Kiongozi huyo katili na mtesaji aliingia madarakani mwaka 1974 wakati alipompindua mjomba wake, Francisco Macias Nguema, kulipiza kisasi cha kiongozi huyo kuua familia yake.

Wapinzani wake ambao wanamshutumu kuwa mlaji wa nyama ya binadamu ameendesha ukandamizaji mkubwa wa mateso na mauaji ya wapinzani wake, akipika na kula viungo vya watu ambao amewaua kwa nia ya kuongeza nguvu zake za kiume.

Severo Moto, mmoja wa wapinzani wa Nguema, mwaka 2004 aliiambia redio moja ya Hispania kuwa kiongozi huyo alithubutu hata kutafuta viungo vya mwili wa Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchi hiyo. “Nasema hivyo kwa sababu Kamishna huyo wa Polisi alizikwa bila kuwa na kende pamoja na ubongo wake.”

Anaongeza Moto, “…anataka na mimi niende Guinea ili aweze kutafuna kende zangu.”

Moto pia anasema kuwa upo ushahidi wa kuthibitisha kuwa Nguema huwachuna ngozi wapinzani wake wakati wakiwa bado hai. “Baada ya kuwa madarakani kwa muda mrefu sana na hasa baada ya kuleweshwa na madaraka hata kama asingekuwa amekaa muda mrefu kiasi hicho sasa anaamini kuwa anazo nguvu na uwezo kama wa Mungu.”

“Anaweza kumwua mtu yeyote katika Equatorial Guinea bila hata kuwepo na ushahidi wowote kuwa mtu huyo amefanya kosa,” anasema Moto.

Mtawala huyo wa Equatorial Guinea ambaye inasemekana kuwa anayo kansa ya tezi dume, tayari anamwandaa mtoto wake wa kiume, Teodoro Nguema Obiang Mangue, 46, kukamata uongozi wa nchi hiyo kumrithi baba yake.

Mtoto huyo, mwizi mkubwa kama baba yake, tayari anakabiliwa na kesi za wizi katika nchi za nje ikiwemo Marekani na Ufaransa na baba yake tayari amemteua kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo na mrithi wa kiti cha Urais cha baba yake.

Mwaka 2012, gazeti la New York Times liliandika kuwa Polisi wa Marekani walikuwa wamekamata mali za Mangue zinazodhaniwa zilipatikana kwa njia ya wizi ama rushwa.

Miongoni mwa mali zilizokamatwa ni vinywaji vya mvinyo vyenye thamani ya dola za Marekani milioni mbili, sawa na sh bilioni 4.480, jengo moja lenye thamani ya dola za Marekani milioni 180, sawa na sh milioni bilioni 403.2 mjini Paris, Ufaransa.

Jengo hilo lenye vyumba 101 lina chumba cha kuangalia sinema, samani (furniture) yenye thamani ya dola za Marekani milioni 50, sawa na sh. bilioni 112, chumba cha kukatia nywele (hair salon), vyumba viwili vya kufanyia mazoezi, klabu ya usiku pamoja na chumba maalumu cha kuogea cha Turkish bath.

Miongoni mwa mali nyingine zilizokamatwa ni pamoja na magari 11 ya kifahari, yakiwemo baadhi ya magari ghali zaidi duniani ikiwa ni pamoja na magari mawili aina ya Nugatti Veyrons na magari aina za Maybach, Aston Martin, Ferrari Enzo, Ferrari 599 GTO, Rolls-Royce Phantom na Maserati MC12.

Mpaka Juni 2013, Wizara ya Sheria ya Marekani ilikuwa inadai kuwa Obiang mtoto alikuwa ametumia kiasi cha dola za Marekani milioni 315, sawa na sh bilioni 705, kununulia mali na vifaa vya anasa kati ya mwaka 2004 na 2011.

Mali hizo zilikuwa ni pamoja na aina za mvinyo zenye thamani kubwa, vinyago vyenye thamani za juu kabisa, saa ya ukutani yenye thamani ya dola za Marekani milioni 3.7, sawa na sh bilioni 8.2, ndege binafsi aina ya Gulfstream Jet, na pia kuwa alikuwa ametumia kiasi cha dola za Marekani milioni mbili, sawa na sh. bilioni 4.4, kununulia bidhaa za ukumbusho za mwanamuziki Michael Jackson.

Kiasi cha fedha ambacho Teodoro hutumia kwenye anasa tu ni sawa na mara tatu zaidi ya kiasi cha fedha ambacho nchi ya Equatorial Guinea hutumia kwa ajili ya bajeti za afya na elimu kwa mwaka.

Pamoja na kwamba Equatorial Guinea ni moja ya nchi 30 zinazoongoza duniani kwa uzalishaji wa mafuta, mtoto anayezaliwa katika nchi hiyo mwaka huu ana nafasi ndogo sana ya kuishi kwa sababu Shirika la Mfuko wa Umoja wa Mataifa la Utamaduni na Elimu (UNICEF) linasema.


Kuwa asilimia 20 ya watoto wanaozaliwa nchini huyo watakufa kabla ya kufikisha umri wa miaka mitano kwa sababu ya hali mbaya ya huduma za afya, tiba, chanjo na hospitali katika nchi hiyo.

Zaidi ya asilimia 60 ya wananchi wote katika Equatorial Guinea wanaishi katika ufukara wa kutupa kwa sababu wastani wa huduma ya afya ni dola za Marekani 60, sawa na sh. 134,400, wastani wa mshahara ni dola za Marekani 186, sawa na sh. 416,640 na zaidi ya nusu ya wakazi wote wa nchi hiyo hawana maji safi na salama ya kunywa.

Transparency International, taasisi ya kimataifa inayofuatia mienendo ya rushwa duniani imeiweka Equatorial Guinea miongoni mwa nchi 12 zinazoongoza kwa rushwa duniani wakati uchunguzi wa Baraza la Seneti la Marekani katika mwenendo wa Benki ya Riggs ya mjini Washington.


Benki hiyo imebaini kuwa familia ya Obianga ilikuwa imepokea hongo nono kutoka katika kampuni za mafuta za Marekani za Exxon Mobile na Amerada Hess.Chanzo/raiamwema.co.tz
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: