Dodoma: Pambano kati ya bondia Francis Cheka na Mmalawi Even Masamba lililopangwa kuchezwa leo kwenye Uwanja wa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma limeota mbawa na sasa Cheka atapigana na Juma Rashid saa 2 usiku mahali hapo hapo.
Pambano hilo ambalo ni la raundi 8 lilipangwa kuanza saa 12 jioni baada ya mapambano ya utangulizi yaliyotarajiwa kuanzia saa 8 mchana.
Akizungumza baada ya kupima uzito, Cheka amesema alijipanga kupigana na Mmalawi huyo lakini kutokana bondia huyo kushindwa kufika atahakikisha anampiga mpinzani wake huyo mpya, Juma Rashid ili kukata kiu ya watakaofika Uwanja wa Jamhuri kushuhudia pambano hilo.
Naye bondia, Juma Rashid aliyetoka Dar es Salaam ametamba kumwangusha Cheka katika raundi ya 3 ili kukomesha umwamba wake kwenye ndondi na pia kuwashangaza watakaotazama pambano hilo.Mwananchi

0 comments:
Post a Comment