BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MATUMAINI YA KUPATA WATU WAKIWA HAI WAFIFIA BAADA YA BWAWA KUBOMOKA NA KUZAA MAAFA

Juhudi za kuwatafuta manusura bado zinaendelea katika eneo ambalo bwawa lilivunja kingo zake na kusababisha maafa makubwa eneo la Nakuru nchini Kenya.

Hata hivyo, matumaini ya kuwapata watu wakiwa hai yanaendelea kudidimia.

Watu 45 walifariki kutokana na mkasa huo uliotokea siku ya Jumatano, karibu na mji wa Solai, kilomita 190 kaskazini magharibi mwa mji kuu Nairobi.

Kuna wasiwasi kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.

Karibu nusu ya waliofariki ni watoto, polisi wamesema.
Uchunguzi wa kisa hicho ulianzishwa rasmi siku ya Ijumaa.

Polisi wanatarajiwa 'kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha bwawa hilo kupasuka'' na kutowa ripoti kamili kwa ya wiki mbili zijazo, afisi ya mwendesha kuu wa mashtaka imesema.
Bwawa lilijengwa kinyume cha sheria

Hayo yamejiri huku mamlaka ya kusimamia maji Kenya ikisema bwawa hilo , pamoja na mabwawa mengine mawili katika shamba hilo la Patel, lilijengwa kinyume cha sheria.

Msemaji wa Mamlaka ya Rasilimali za Maji (Warma) Elizabeth Luvonga ameambia shirika la habari la Reuters kwamba bwawa hilo lilijengwa bila idhini inayohitajika kutoka kwa serikali.

"Hakuna bwawa hata moja lililo na hati ya idhini. Ndio maana ni haramu," amesema.

Lakini msimamizi wa shamba hilo Vinoj Kumar amekanusha tuhuma hizo.

"Mabwawa haya yalijengwa miaka 15 hadi 20 iliyopita. Hakuna chochote kilichofanywa kinyume cha sharia," amesema. Watu zaidi ya 2,000 waliachwa bila makao baada ya nyumba zao kuharibiwa na maji kutoka kwa bwawa hilo

Bwawa hilo lilivunja kingo zake mwendo wa saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki ((18:00 GMT) siku ya Jumatano na kutoa zaidi ya lita 70 milioni za maji.

Maji hayo yalipitia kwenye vijiji viwili na kusomba watu, mali na mifugo. Maji ya bwawa hilo yalichimba ufa ardhini

Kilingana na gazeti la Daily Nation la Kenya, kina cha maji yaliyovunja kutoka kwa bwawa hilo kilikuwa zaidi ya mita moja na unusu na maji hayo yalipitia eneo la upana wa mita 500.

Bwawa hilo kiliharibu kila kitu kwenye njia yake - ikiwemo shule moja ya msingi na nyaya za kusambaza umeme.
'Niling'ang'ania mtini'

''Maji yalifurika kwa kasi sana,'' Josephat Kimeli, mmoja wa walionusurika ameiambia BBC . ''Nilipokuwa nikijaribu kukimbia, watoto wangu wawili wa kike walibebwa na maji hayo.

''Niliweza kumuokoa mke wangu na watoto wavulana wawili. Lakini kwa hivi sasa nina uchungu mwingi: Uchungu wa kuwapoteza watoto wangu.''

Ngugi Njoroge, mmoja wa wakaziwanaopata matibabu baada ya kupata majeraha, amewaambia wanahabari kutoka kwa kitanda cha hospitali kwamba alitenganishwa na familia yake.

''Nilikuwa na wazazi wangu na ndugu yangu wa kiume,'' alisema. „Sijui walipo: Nilibebwa na maji lakini nilibahatika nilipong'ang'ania mti hadi pale maji yalipopungua."
Gavana wa jimbo hilo la Nakuru , Lee Kinyanjui amesema watu 40 wameripotiwa kupotea na bado hawajapatikana. Na wengine 44 wamethibitishwa kufariki, aliongeza.

Bwawa hilo lililoko kwenye shamba binafsi na ambalo linadaiwa kutumiwa kunyunyuzia maji mimea yake lilivunja kingo zake kutokana na mvua kubwa iliyoshuhudiwa katika eneo hilo Jumatano.

Mvua kubwa iliendelea kunyesha Alhamisi na Ijumaa na kutatiza juhudi za uokoaji.

Kuna wasiwasi kuhusu mabwawa mengine katika eneo hilo, mawili yakiwa katika shamba hilo la mwanabiashara anayefahamika kama Patel.

Bw Kinyanjui alitoa tahadhari kwamba lazima bwawa moja 'lifunguliwe maji yapunguzwe ili kujiepusha na janga jingine.''

Maafisa wa jeshi walichukua hatua Ijumaa na kuanza kupunguza maji katika bwawa hilo moja.

Awali, taarifa zilienea kwamba bwawa hilo lilikuwa linavunja kingo zake lakini baadaye serikali ikafafanua kwamba maji ni maafisa wa jeshi na maafisa wengine wa serikali waliokuwa wakiyafungulia maji na kuyaondoa kwa utaratibu.

Kabla siku ya Juamtano, watu 132 walikuwa wamefariki kote nchini humo kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha maeneo mengi nchini humo tangu mwezi Machi.

Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya linasema takriban watu 300,000 kufikia sasa wamelazimika kuyakimbia makwao kutokana na mvua.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: