KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR.
Juma Mtanda, Morogoro.
Kocha Mkuu wa klabu ya Mtibwa Sugar, Zubery Katwila amewaomba mashabiki na wadau mbalimbali wa soka mkoani Morogoro kuisapoti timu hiyo wakati wa fainali ya kombe la FA ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la shrikisho barani afrika.
Mtibwa Sugar ilitinga fainali ya FA baada ya kuitandika Stend United bao 2-0 kwenye uwanja wa CCM Kambarage na kufuzu kuingia fainali ya kombe hilo huku kwenye mchezo wa robo fainali ikiitoa Azam FC.
Akizugumza na gazeti hili mjini hapa, Katwila amesema kuwa wachezaji wake wana morali kubwa na mchezo wa fainali na ili kutimiza ndoto ya kutwaa kombe hilo na kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani wanahitaji maombi.
Katwila amesema kuwa benchi la ufundi, wachezaji na wanachama wana lengo moja tu la kutwaa kombe la FA dhidi ya Singida United huku wakiwapigia magoti wadau mbalimbali wa soka na mkoa wa Morogoro kiujumla kujitoa mhanga kwenda kuwashangilia kwenye mchezo wa fainali kati ya Singida United au JKT Tanzania.
“Jambo la kwanza tunawaoma wadau mbalimbali wa soka na mashabiki wetu kuanza kujiandaa na safari ya kwenda kuishangilia kwa ari na mali kwenye mchezo wao wa fainali kati ya Singida United ama JKT Tanzania utaopangwa baadaye ili nasi tuweze kupata morali ya juu hatimaye kurudi na kombe la FA Morogoro.”alisema Katwila.
Aliongeza kwa kusema kuwa Mtibwa Sugar haijatwaa kombe kipindi kirefu hivyo kuingia fainali ya FA kumeifanya kufufua ndoto yao ya kutwaa kombe hilo ili kuiwakilisha nchi michezo ya kimataifa.
“Mtibwa Sugar ilitwaa makombe ya ligi kuu tanzania bara mwaka 1999 na 2002 chini ya kocha wake, John Simkoko na makombe mengine likiwemo la Tusker sasa na sasa yupo kocha mkuu, Zubery Katwila kuweka historia ya Mtibwa Sugar kutwaa kombe la FA na tuna kiu na kombe hili.”alisema Katwila.
Katwila amesema kuwa wachezaji wawili, Shabaan Nditi na Dickson Daud ndio waliopata bahati ya kutwaa kombe Mtibwa Sugar la Tusker na kuwaomba wadau wa soka kuwaombea dua njema ili kupata ushindi kwenye mchezo wa fainali.
Wakazi wa mkoa wa Morogoro wamemisi mashindano ya kimataifa kutokana na Mtibwa Sugar kushindwa kutwaa kombe la ligi kuu Tanzania bara au kupata nafasi ya kushiriki kombe la shirikisho kwa miaka mingi inayotoa nafasi ya timu kushiriki mashindano ya kimataifa.

0 comments:
Post a Comment