BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DC KILOMBERO, WALEMAVU WANA HAKI YA KUPATA ELIMU

Mkuu wa wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro, James Ihunyo kulia na Amon Mwambasi wakimnyanyua mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi Lufulu kata ya Ching'anda, Ezra Mwambasi (12) kumweka katika baiskeli ya magurudumu matatu baada ya kupata msaada kutoka kwa mwandishi wa gazeti la Mwananchi Morogoro, Juma Mtanda kwa kushirikiana na marafiki na kutoa vifaa vya shule vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh350,000 katika hafla fupi iliyofanyika shuleni.

KILOMBERO. Mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi Lufulu, wilayani Kilombero ambaye ni mlemavu Ezra Amon Mwambasi, pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha bado ameonekana kufanya vyema kitaaluma.

Mwanafunzi huyo pamoja na kuonekana kuishi katika mazingira yasiyo rafiki, lakini bado hali imepelekea kushika nafasi ya nane kwenye matokeo ya wilaya katika mtihani wa taifa wa darasa la nne na kuingia darasa la tano kwa mwaka 2017 Kilombero mkoani Morogoro.

Akizungumza na wananchi katika hafla ya kukabidhiwa baiskeli ya magurudumu matatu kwa mwanafunzi huyo mwenye ulemavu shuleni hapo jana, Mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo, alisema watu wenye ulemavu wana haki ya kupata huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu.

Ihunyo aliwataka wazazi wenye watoto wenye ulemavu kuhakikisha wanawapeleka shule ili wapata elimu, na kuacha tabia ya kuwafungia majumani.

Alisema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wazazi kuwaficha watoto wenye ulemavu huku akiwasihi kujifunza ujasiri wa kukabiliana na mambo mbalimbali yanayotokea katika familia.

“Angalieni kama wazazi wa Ezra wangeamua kumfungia mtoto wao ingekuwaje, waliamua kumpeleka shule na leo ameonyesha kipaji kikubwa darasani licha ya changomoto zinazomkabili,”alisema Ihunyo.

Mkuu huyo wa wilaya alikabidhi baiskeli hiyo ilitolewa na mwandishi wa gazeti hili la mwananchi na vifaa vya shule kwa kushikiriana na marafiki vyenye thamani ya zaidi ya sh 350,000.

“Niwapongeze wazazi wa Ezra Mwambasi kwa kitendo chenu cha kumpeleka shule lakini niwaombe wananchi wote wa eneo hili na wilaya hii msiwe na tabia ya kuwaficha majumbani watoto wenu walemavu, ”alisema Ihunyo.

Ezra Mwambasi (12) akizungumza mara baada ya kupokea baiskeli hiyo alisema baiskeli hiyo itamsaidia kusafiri na hata kwenda shule kwa wakati, kuwatembelea marafiki na kuitumia kwenda kwenye katika mitihani ya shule ya ujirani mwema ambayo alisema alikuwa akiikosa kwa muda mrefu.

“Nashukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata msaada huu wa baiskeli kwani itanirahisishia kutoka nyumba kwenda shule na maeneo mengine

lakini pongezi ya pekee ni kwa rafiki yangun Juma Mtanda na marafiki zake kwa kupata wazo la kuniwezesha upatikaji wa baiskeli,”alisema Ezra.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Lufulu, Fadhil Mkhoi alisema kuwa mwanafunzi huyo amekuwa mwenye kuonyesha juhudi kubwa darasani kwa kufanya vyema kitaaluma tangu akiwa shule ya awali na kuendelea kushikaa nafasi ya kwanza hadi msingi.

“Kuna changamoto nyingi za kimazingira zimejitokeza ama anakabiliana nazo mwanafunzi huyu ikiwemo kutokuwepo vyoo vya maalumu lakini hilo halijawa kikwazo kwake la kumrudisha nyuma kimasomo,”alisema Mkhoi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: