BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Kipa wa soka 'asingizia jereha' ili aweze kufungua mwezi wa Ramadhan

Kikosi cha kombe la dunia cha Tunisia kimepata njia ya kukabiliana na uchovu huku wakiendelea kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Katika mechi za kirafiki dhidi ya Ureno , aliyekuwa kipa wa Uturuki, Mouez Hassen alionekana kusingizia jeraha wakati funga hiyo ilipokamilika saa za jioni.

Alipokuwa akilala uwanjani ili kupata matibabu , wachezaji wenzake walikimbia hadi nje ya uwanja ili kunywa maji na tende.

Na hatua hiyo ilileta matokeo. Wakiwa nyuma 2-1 dhidi ya mabingwa wa Ulaya 2-1 Ureno, Tunisia walisawazisha dakika sita baada ya jeraha la Hassen na hivyobasi kumaliza mechi hiyo ikiwa 2-2.

Siku chache baadaye dhidi ya Uturuki, Hassen alisitisha mchezo kwa kulalia mgongo wake.

Kwa mara nyengine wachezaji wenzake walikula tende na kunywa maji waliyopewa na wahudumu wa kitendo cha ukufunzi . Mechi hiyo ilikwisha 2-2. Beki Ali Maaloul (L) anaonekana hapa akila tende Na baadaye anachukua tama la maji alilopewa na muhudumu wa kitengo cha ukufunzi.

Wachanganuzi nchini Tunisia kwa haraka walichunguza wakati kipa huyo aliposingizia kuumia katika mechi zote mbili katika dakika ya 58 na 47 mtawalia.

Muda huo uliingiana na muda wa Iftar ambapo Waislamu hufungua mwezi wa Ramadhan kwa kula tende na maji. Shirikisho la soka nchini Tunisia bado halijazungumzia kuhusu mapumziko hayo ya jeraha.

Lakini kipa Hassan alituma ujumbe wa Twitter: ''Niliumizwa, [akiweka emoji za kucheka]' akimjibu mchezaji mwenza Chaker Alhadhurt aliyejibu: ''Ni sawa sasa tunajua ulikuwa aukidanganya''

Haipatikani tena
Macho yote sasa yatakuwa yakimlenga kipa wa Tunisia wakati timu hiyo itakapocheza mechi nyengine ya kirafiki dhidi ya Uhispania tarehe 9 Juni.

Mechi ya kwanza ya kombe la dunia dhidi ya timu hiyo ya Afrika kaskazini itafanyika Uingereza Juni 18 wakati ambapo Ramadhana itakuwa imekamilika. Tunisia ni miongoni mwa timu tamno za Afrika katika kombe la dunia
 

Ramadhan ni nini?
Wakati wa Ramadhan, Waislamu hutakiwa kutokula chakula, maji na kutoshiriki katika tendo la ngono kutoka alfajiri hadi jioni.

Lengo lake ni kufanya ibada na kujizuia .Nia ya kutaka kufunga lazima ifanywe usiku kabla ya mtu kulala ama wakati wa chakula cha daku.

Inaruhusiwa kutofunga wakati wa Ramadhan miongoni mwa Waislamu iwapo mtu ana tatizo la kiakili, anahisi kiu kikali, anasafiri ama iwapo maisha yako yapo hatarani iwapo hutafungua.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: