Juma Mtanda, Morogoro.
Morogoro. Kesi ya jinai inayowakabili wabunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga, Peter Lijualikali wa jimbo la Kilombero na wenzao 11 imeahilishwa hadi Julai 5 mwaka huu.
Kesi hiyo imeahilishwa kufuatia wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala kuwasilisha barua ya kuomba kesi hiyo isogezwe mbele inayosikilizwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro na, Ivan Msack kutokana na majukumu mengine.
Akizungumza na wafuasi, wanachama na ndugu wa washtakiwa nje ya mahakama hiyo juzi, Mbunge wa jimbo la Mlimba, Suzan Kiwanga aliwaeleza kuwa mahakama ilipanga kusikiliza kesi hiyo leo kwa mashahidi upande wa jamhuri kutoa ushahidi lakini kesi imeghailishwa hadi Julai 5.
Tayari mashahidi wawili wametoa ushahidi kwa mashtakiwa hao kati ya mashahidi 20 wa upande wa mashtaka.
Kiwanga alisema kuwa kesi hiyo itasikilizwa mfululizo Julai 5, 6 mwaka huu huku upande wa mashtaka ikipeleka mashahidi sita.
“Niwaombe ndugu zangu muonyeshe moyo wa kutusapoti kwa kuja mahakamani tena Julai 5 na 6 ambao itasikilizwa tena mfululizo kwa mashahidi upande wa jamhuri kutoa ushahidi lakini wakili wetu, Peter Kibatala amewasilisha barua mahakamani ya kuomba kughailisha na imeridhia hadi tarehe iliyopangwa.”alisema Kiwanga.
Hata hivyo, upande wa mashtaka umeomba mahakama kuridhia ombi lao la kuongeza mashataka mengine nane baada ya awali nane na sasa yamefikia mashtaka16.
Mahakama hiyo tayari imesikiliza ushahidi wa mashahidi wawili ambao ni Mkurugenzi wa Halmashahiri ya Malinyi, Maseline Ndimbwa na afisa Mtendaji kata ya Sofi.
Ushahidi wa kwanza katika kesi hiyo ilianza kusikilizwa Mei 18 mwaka huu huku ikipangwa kusikiliza tena leo Juni 7.
0 comments:
Post a Comment