Miili ya pacha walioungana Maria, Consolata yaanza kuagwa Iringa
Miili ya pacha walioungana Maria na Consolata imewasili kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha Iringa (Rucu).
Tukio la kuagwa kwa pacha hao limetangazwa kuwa ni la kitaifa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ameeleza kuwa Rais John Magufuli ni miongoni mwa walioguswa na kuhuzunishwa na vifo hivyo.
"Huu ni msiba wa kitaifa Rais angehudhuria ila amebanwa na ratiba Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Sera, Bunge na Walemavu, Stella Ikupa wataudhuria hapa," amesema Kasesela.
Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo, Abdul-Razaq Badru ni miongoni mwa watu waliohudhuria akaeleza kusikitishwa na vifo hivyo kwa kuwa vimezuia pacha hao kutotimiza ndoto zao za kuwa wanataaluma.
Anatumia nafasi Hiyo kuwasihi wanafunzi kutambua mikopo inayotolewa ni rasilimali muhimu, Serikali inalenga kuwawezesha ili wawe wataalam watakaosaidia nchi.
0 comments:
Post a Comment