BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU 10 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA KUTOKEA AJALI YA TRENI NA BASI LA ABIRIA KIGOMA

Watu 10 wamefariki katika ajali iliyotokea baada ya basi la abiria lililogongana na treni eneo la Gungu katika manispaa ya Kigoma Ujiji, kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 12:15 asubuhi leo.

Basi hilo la abiria ambalo linamilikiwa na kampuni ya Prince Hamida linadaiwa kugongana na treni lilipokuwa linatoka Kigoma Mjini kwenda Tabora.

Treni hiyo ya mizigo ilikuwa ikitoka Kazuramimba kwenda Kigoma Mjini.

Rais wa Tanzania John Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kuwtaaka „wadau wote wa usalama barabarani kuchukua hatua madhubuti za kuzuia ajali hizi."

"Vyombo husika, chukueni hatua kali kwa wote wanaokiuka sheria za usalama barabarani," amesema.

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema eneo ilipotokea ajali hiyo hutokea ajali za aina hiyo mara kwa mara.

"Nimezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania ( TRC ) na tumekubaliana kuwa tuweke kizuizi ( barrier ) Katika eneo hili ambapo reli ikatiza barabara," amesema.

„ Hii itasaidia sana kupunguza ajali za namna hii. Mkurugenzi wa TRC Bwana Masanja Kadogosa amekubali ushauri huu ambao Wananchi wengi wa Kigoma Mjini wamekuwa wakiutoa."
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: