BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SHULE KUKABILIWA NA UHABA WA MADAWATI

SHULE ya msingi Misufini A iliyopo kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro inakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo upungufu wa madawati 125 ambayo yaliharibika baada ya kudondokewa na paa.


Akizungumzia na mwandishi wa habari hii kuhusu tukio hilo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Jane Mlangwa alisema uharibifu huo wa madawati 125 ulitokana na mvua iliyoambata na upepo mkali ulioezua paa katika vyumba tisa vya madarasa ya shule hiyo.


Mlangwa alisema kuwa mahitaji ya madawati kwa sasa ni makubwa hasa kwa wanafunzi wa darasa la pili na tatu ambapo kwa sasa wanalazimika kutumia dawati moja kwa wananfunzi wanne badala ya dawati moja kukaliwa na wanafunzi wawili na madarasa menginine ambayo yamekuwa na upungufu huo.


Alitaja matatizo mengine yanayoikabili shule hiyo baada ya kutokea kwa athari hizo ambapo unahitaji kufanyike ukarabati wa milango, madirisha, kupiga rangi kuta za vyumba tisa vya madarasa hayo kati ya vyumba 18 vilivyoezuliwa ambapo vibaka wamekuwa wakitumia mwaya huyo kuiba vifaa vya shule na baada ya kumaliza kazi hiyo wamekuwa na tabia ya kujisaidia haja kubwa na mdogo ndani ya baadhi ya vyumba vya madarasa.


“Kwa kweli ratiba ya masomo ilibadilika kwa kipindi kile cha mwezi mmoja hali ambayo ilisababisha wanafunzi kurundikana kwenye darasa moja kwa mikondo minne iliyokuwepo kwa kila darasa hali hiyo ilisababisha kutumia dawati moja kukaa wanafunzi wanne badala ya wawili kwa dawati moja kwa kipindi cha mwezi wa pili yalipotokea maafa hayo,” alisema Mlangwa.


Pia hali hiyo ililazimu wanafunzi kusoma kwa mikondo miwili ya darasa la kwanza A na B katika darasa mmoja na mikondo miwili ya darasa la tatu A na B.


Alisema kuwa wataalam wa Manispaa ya Morogoro walifanya tathimini ya athari hiyo ya ambapo jumla ya mali zenye thamani ya Sh36 milioni ziliharibika ambapo kiasi hicho kinahitajika ili kukidhi mapungufu yaliyopo.


Baada ya kupata janga hilo kamati ya shule hiyo ilikaa na kuanza kuandika barua kwa wafadhili mbalimbali ili kuweza kujitokeza kusaidia upatikanaji wa Sh36.6 milioni na hadi sasa jumla ya Sh23.6 milioni zimepatikana.


Kuhusu upungufu wa vitabu shuleni hapo mwalimu mkuu huyo alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa vitabu kwa darasa la kwanza hadi darasa la tatu ambapo kwa sasa kitabu kimoja hutumiwa na mwanafunzi watatu badala ya mahitaji ya kitabu kimoja kwa mwanafunzi mmoja kulingana na malengo ya taifa.


Mlangwa aliwataja wafadhili waliojitokeza kusadia msaada wa vifaa na fedha taslimu kuwa ni pamoja na benki ya NMB mbayo imetoa mbao zenye thamani ya sh 6,000,000, PPF ambayo imetoa mifuko ya saruji 70 ikiwa na thamani ya sh 1,080,000, Kiwanda cha Tumbaku (TTPL) kimetoa vitabu vya kiada na ziada kwa darasa la tano na sita vyote vikiwa na thamani ya sh 6,372,000 milioni.


Wengine ni pamoja na Waziri wa Fedha, Msatafa Mkulo sh 500,000, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro sh 7,475,000 milioni, Wazazi wa shule hiyo sh 400,000 na Baraza la Maendeleo ya kata Mafiga sh 500,000 ambazo zote hizo zikiwa na jumla ya 22,327,000 milioni.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: