BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MABINGWA WA SOKA MKOA WA MOROGORO YAANZA VEMA MASHINDANO YA MEI MOSI MORO.


Mchezaji wa timu ya soka ya Tumbaku Fc Haji Mfaume mbele akijaribu kumtoka mchezaji wa Ukagauzi Juma Msukule nyuma wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Mei Mosi katika uwanja wa Jmahuri mjini Morogoro ambapo katika mchezo huo Tumbaku Fc waliibuka na ushindi wa bao 4-3.




MABINGWA wa soka mkoa wa Morogoro timu ya Tumbaku FC imeanza vema mashindano ya kuwania ubingwa wa Mei Mosi baada ya kufanikiwa kuitandika timu ya Ukaguzi katika mchezo mkali na wakusisimua katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo yaliyoanza kutimua vumbi April 16 kwa bao 4-3 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Dalili za mabingwa hao kuibuka na ushindi zilianza mapema baada ya mshambuliaji wao, Mohamedi Yusuph kuiandikia bao la kuongoza dakika ya saba kufuatia kuonana vizuri safu ya ushambuliaji kwa timu hiyo ya Tumbaku Fc na kutoa mwanya wa kufunga bao.

Baada ya timu ya Ukaguzi kufungwa bao hilo ilianza kucheza mchezo wa kusaka bao la kusawazisha kwa kushambulia kwa kustukiza na dakika ya 27 walipata bao lililofungwa na, RidhaaAbeid kwa njia ya penalti kufuatia kuangushwa kwa mshambuliaji wao eneo la hatari na mlinzi wa Tumbaku Fc, Deo Protas na mwamuzi wa mchezo huo, Seleman Kinugani aliamuru ipigwe adhabu hiyo.

Kuingia kwa bao hilo timu ya Ukaguzi ilianza kujiamini na kuchezo mchezo mzuri hasa katika safu ya kiungo na ushambuliaji kwa kucheza pasi fupi fupi na dakika ya 65 walipata bao la pili ambalo lilifungwa kiufundi na Benard Chezuwe.

Bao hilo la Ukaguzi lilidumu hadi dakika ya mbili ambapo katika dakika ya 67mabingwa hao wa mkoa wa Morogoro Tumbaku Fc walizawazisha bao hilo na matokea kufanya bao 2-2 hadi katika dakika hiyo.

Timu ya Ukaguzi ambayo muda mwingi ilikuwa inashambuliwa na wapinzani wao ilikuwa ikitumia zaidi mashmbulizi ya kustukiza ambapo katika dakika ya 81 iliweza kupata bao la tatu kupitia kwa, Hamisi Juma aliyekuwa akisumbua gombe ya Tumbaku kutokana na mfumo huo baada ya kutanguliziwa mpira na, Riadhaa Abeid.

Mashabiki waliohudhuria mchezo huo wa ufunguzi wakianza kutoka uwanjani hapo huku wakiamini Ukaguzi ingeweza kuibuka na ushindi huo nahonda wa timu ya Tumbaku Fc Julius Tindwa alibadilisha matokea katika dakika ya 87 kwa kupachika bao la tatu kwa timu yake na kusawazisha baada ya kuvumua mpira wa chini ulioenda moja kwa moja na kujaa wavuni katika lango la Ukaguzi.

Katika dakika ya 90 mchezaji wa timu ya Tumbaku Fc alifanyiwa madhambi nje kidogo ya 18 na mlinzi wa Ukaguzi na mwamuzi wa mchezo huo Selaman Kinugani aliamuru ipigwe adhabu hiyo ambayo ilipigwa kiufundi na Isdoly Katula ambapo mpira huo ulijaa wavuni katika lango la Ukaguzi na matokeo ya mchezo huo kufanya Tumbaku Fc kuibuka na ushindi wa bao 4-3.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: