TIMU ya Netiboli ya Polisi Tanzania imenza mashindano ya Mei Mosi kwa kutoa kuichapa timu ya Chuo cha Mipango Dodoma (IRDP) kwa kuifunga mabao 50-4 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Akinadada wa timu ya Polisi Tanzania ambao walionekana mapema kuwapania katika mchezo huo walianza kupata mabao ya mapema kupitia kwa wafungaji wao mahili Aziza Itonya ambaye alifunga bao 11 na Fatuma Chanzi aliyefunga mabao 8 katika ngwe ya kwanza na kufanya kumaliza wakiwa na mabao 19 dhidi ya mabao mawili ya wapinzania wao.
Mabao ya timu ya Chuo cha Mipango Dodoma (IRDP) yalitumbukizwa kwenye wavu na washambuliaji wao tegemeo Rabia Mrisho aliyefunga bao moja na Eva Semazua naye akifunga bao moja kwenye mchezo huo ambao walihelemewa kila idara.
Wakitumia uzoefu kwenye mchezo huo wachezaji wa timu ya Polisi Tanzania walendelea kutawala mchezo huo katika kila idara hali ambayo iliwapa wachezaji hao kutengeneza nafasi nyingi za mabao ddhidi ya wapinzania hao ambapo kwenye ngwe ya pili Fatuma Chanzi aliweza kuifungia timu yake maabao 17 wakati Aziza Itonya naye akifunga mabao 14 na kumaliza wakiwa na idadi ya mabao 31 dhidi ya timu ya Chuo cha Mipango Dodoma (IRDP) iliyofunga mabao mawili.
Mabao ya timu ya Chuo cha Mipango Dodoma (IRDP) yalifungwa na wafungaji wao Rabia Mrisho aliyefunga bao moja na Eva Semazua naye akifunga bao moja.
Katika michezo mingine iliyochezwa kwenye uwanja huo timu ya akinadada wa Alliance One ilibuka na ushindi wa mabao 27 dhidi ya timu ya Hazina ambayo iliambulia mabao 11 ambapo michezo mingine itaendeelea kwenye uwanja wa huo wa Jamhuri mjini hapa.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / TIMU YA NETIBOLI YA POLISI TANZANIA YAANZA NA KIBONDE MASHINDANO YA MEI MOSI MORO.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment